Naiona Super Cup ya Yanga vs Mamelod Sundowns hapo mwakani

Natafuta Ajira

JF-Expert Member
Mar 25, 2020
4,417
9,806
Kwanza kabisa kama ikiwapendeza FIFA kwa mwaka huu World Cup isifanyike maana wananchi washamaliza burudani yote. Hivi tutarajie kuona nini kingine kutoka kwa kina Messi, Neymar, Mane, De Bruyne ambacho hatukukiona jana pale Tunisia? Nitajie kimoja tu?

Twende kwenye mada husika. Nimeangalia timu zote zilizofuzu sioni timu yoyote ya kuwasumbua wananchi huku confederation. Najua watu watasema hatua ya mtoano itawagharimu wananchi maana hawafungi magoli ya kutosha nyumbani na hii ni sababu kwa kawaida tulishazoea timu inalinda 'away' kwa kutegemea kwenda kushinda nyumbani.

Ila wananchi chini ya Professor Nabi wamekuja na utamaduni mpya, yaani unapigiwa mpira mkubwa kwako na ugenini. Kama unabisha waulize Al Hilal waliopaki basi dakika 180 na Club Africain, kwaiyo kwa wapinzani wa Yanga uko CAF kupata sare kwa Mkapa siyo suluhisho.

Kwa kule CAF Champions League nawapa nafasi zaidi Mamelod Sundowns. Mwakani naiona kabisa CAF Super Cup ya Yanga dhidi ya Mamelod Sundowns.
 
hiyo mechi ya supercup yanga 3-mamelod 1,baada ya hapo tutauza fei kwa b4,aziz kwa b6,mayele kwa b4
 
Tutasikia mengi baada ya yanga kuonja makundi.
Inabid tuwavumilie tu maana hatuna jinsi ,so utopolo tambeni tu bandugu ,Ila mpira wa huko kimataifa sio sawa na wabongo ,una mikakati mingi Sana.
Kumtoa mwarabu kusiwape kichwa Sana had kujiona mshamaliza kila kitu.
Nasemaje tambeni tu maana maskin akipata mtaa mzima utajua tu.
 
Tutasikia mengi baada ya yanga kuonja makundi.
Inabid tuwavumilie tu maana hatuna jinsi ,so utopolo tambeni tu bandugu ,Ila mpira wa huko kimataifa sio sawa na abongo ,una mikakati mingi Sana.
Kumtoa mwarabu kusiwape kichwa Sana had kujiona mshamaliza kila kitu.
Nasemaje tambeni tu maana maskin akipata mtaa mzima utajua tu.
Tumejipanga mkuu ndoo lazima ije bongo ondoa mashaka.. tunaenda kuondoa ule utaratibu wa kushangilia kumaliza robo fainali
 
Kwanza kabisa kama ikiwapendeza FIFA kwa mwaka huu World Cup isifanyike maana wananchi washamaliza burudani yote. Hivi tutarajie kuona nini kingine kutoka kwa kina Messi, Neymar, Mane, De Bruyne ambacho hatukukiona jana pale Tunisia? Nitajie kimoja tu?

Twende kwenye mada husika. Nimeangalia timu zote zilizofuzu sioni timu yoyote ya kuwasumbua wananchi huku confederation. Najua watu watasema hatua ya mtoano itawagharimu wananchi maana hawafungi magoli ya kutosha nyumbani na hii ni sababu kwa kawaida tulishazoea timu inalinda 'away' kwa kutegemea kwenda kushinda nyumbani.

Ila wananchi chini ya Professor Nabi wamekuja na utamaduni mpya, yaani unapigiwa mpira mkubwa kwako na ugenini. Kama unabisha waulize Al Hilal waliopaki basi dakika 180 na Club Africain, kwaiyo kwa wapinzani wa Yanga uko CAF kupata sare kwa Mkapa siyo suluhisho.

Kwa kule CAF Champions League nawapa nafasi zaidi Mamelod Sundowns. Mwakani naiona kabisa CAF Super Cup ya Yanga dhidi ya Mamelod Sundowns.

Screenshot_20221113-172010.png

kabla ya kucheck world cup tungeicheck hii documentary ingekuwa bora sana yani.
 
Back
Top Bottom