Naiona Safari yangu ya Kuwa Tajiri!

Naiona Safari yangu ya Kuwa Tajiri!

Kila la heri mkuu... Na ukiona unahitaji nguvu kazi ya kukupa sapoti tupo hapa usisite kutushirikisha
 
Changamoto ni nyingi sana utakutana nazo hapo mbele mkuu, muhimu kukaza.

Pia baada ya kufanikiwa usijipe tumaini kwamba nishafika peak, mambo yanageukaga watu wameshika mpaka B4 saivi hawana hata uhakika wa mlo mmoja.

Pitia ule uzi wa “tuliowahi kushika pesa na tukafilisika” utakujenga kwa namna flani positive na kuna mwingine tena ”tuliowahi kuchukua mikopo na hatukufanyia vitu vya maana”

Mungu ni mwema tupo katika njia moja.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mungu ni mwema siku zote!
Nilianza chuo hapa dar es salaam(chuo Fulani)

Tangu naanza chuo mpaka nimepostpone mwaka wa Pili sikuwai kutumia pesa ya Boom!

Nilikuwa najihusisha na uvuvi, kuuza mtumba kuuza samaki nk.
Ndoto Zangu Ni kufanikiwa kupitia vyombo ya usafiri!

Sasa baada ya kupata hiyo fedha! Nimeenda bank kuchukua mkopo wa Bajaj! Nina uhakika baada ya mwaka mmoja nitamaliza mkataba.

Na Nina uhakika nitakopa kadri ya uwezo wangu!

Nimefanikiwa kununua heka Tano za shamba huko mkoani Tabora!

Malengo yangu mwaka huu nilime heka Tano za mpunga!

Pesa nitakayo ipata kwenye kilimo! Kinachofuata Ni kufungua duka la huduma za kifedha. Airtel money! Bank nk.

Baada ya hapo! Nimepata connection ya fundi wa vitanda vya mninga! Huko Tabora huko anauza laki mbili na nusu!

Vile vitanda huku dar naweza kuuza hata laki Saba.

Shemeji yenu Ni supportive Sana na ananipenda!

Pia hapo badae nitakuwa natoa samaki kambale naleta dar.

Yani Mambo Ni mengi Sana muda mchache.
Naiona Safari yangu ya Kuwa Tajiri

Chuo ntarudi mwakani
Ushauri wowote.
Kwani usikiagi ukiambiwa mipango haiwekwi hadharani mkuu...

Ila kila la kheri.
 
Changamoto ni nyingi sana utakutana nazo hapo mbele mkuu, muhimu kukaza.

Pia baada ya kufanikiwa usijipe tumaini kwamba nishafika peak, mambo yanageukaga watu wameshika mpaka B4 saivi hawana hata uhakika wa mlo mmoja.

Pitia ule uzi wa “tuliowahi kushika pesa na tukafilisika” utakujenga kwa namna flani positive na kuna mwingine tena ”tuliowahi kuchukua mikopo na hatukufanyia vitu vya maana”

Mungu ni mwema tupo katika njia moja.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nashukuru Sana Mkuu
 
Back
Top Bottom