Haihitaji akili nyingi sana kujua hili, ni wazi na ni dhahiri kabisa kuwa hali ya Nchi ni mbaya sana kwa sasa, kitendo cha Wabunge wote wa CCM na wa vyama vyote vya upinzani kuunga hoja Mkono kwa asilimia 100 ya kwamba Mh Makonda Aitwe na kwenda kujitetea Ktk kamati ya maadili bungeni wakati huo huo Akiwa anaungwa Mkono na kusifiwa sana na Raisi ni Dhahiri kuwa wabunge wote hawamuungi Mkono Raisi.
Kwa mitaani hali ni mbaya Zaidi, kila mtu anamzungumzia Makonda kwa Ubaya, siyo Maprofesa siyo Madoctor siyo Machinga, Wasanii ndiyo Kabisa usiseme. Hasa ukizingatia ile Amri yake ya kuzuia Shughuli zote za Burundani kuanzia Saa sita usiku. Amri ambayo imewafanya Wasanii wengi kukosa kazi ya kufanya kwa sababu Hakuna ukumbi unaokubali kuwaalika Wasanii kutumbuiza kwa masaa mawili tu hatafu walipwe, kwa hiyo wengi Kama siyo wote hawana kazi ya kufanya na hali zao ni mbaya sana kifedha.
Wahudumu wa Bar, Kama Watanzania masikini nao pia wana kilio kikali na Wanaongea kila lililo baya kwa Mkuu huyu wa Mkoa, sababu, bar zote zimepunguza wahudumu kwa zaidi ya 80% hii ni kwa sababu wale waliokuwa wakiingia Shift za asubuhi, wote wamepoteza kazi outomatic, na wale wa shift ya usiku wamepunguzwa kwa 50%. Jaribu kuona ni familia ngapi zimeathirika,
Wamiliki wa Mabaa na Maclabu, kila mtu analaani kwa Lugha yake, sababu, masaa ya kufanya kazi ni machache sana, hivyo kufanya Mapato Yao kushuka kwa Zaidi ya 60% bajaji boda boda, na Tax ndiyo balaa, wao walikuwa wakipata abiria kuanzia Asubuhi mpaka usiku saa kumi, sasa hivi wanalazimika kufunga shughuli zao saa sita usiku na kuzifungua saa kumi jioni, Muda mwingi wanautumia kucheza Drafti na kupiga soga zisizo na faida yoyote. Mapato Yao yameshuka kwa zaidi ya 65%
Kutokana na pia Hali za watu za uchumi kuwa mbaya sana, watu wamekuwa na Hasira na Chuki Sana, kuna mpasuko mkubwa sana wa kiuongozi, Wenyeviti wa Serikali za mitaa kila Mmoja analaani kwa Lugha yake.
Je, tutaachana Vipi na hii hali halisi iliyopo ambapo kila Mtu amepoteza Matumaini, Wakati wa Kampeni Wagombea waliahidi kuwa awamu hii itakiwa ni TANZANIA YA VIWANDA. Juzi Waziri wa viwanda amewachana wananchi wazi kuwa, Serikali haina uwezo wa kujenga viwanda ila itaandaa mazingira ya wanachi kujijengea Viwanda. Japo hakufafanua, ila kwa wenye akili timamu tumejua imetoka hiyo!
Wanasiasa wanakamatwa na kufungwa hovyo, yaani ni Chuki kila mahali. Watu wamekosa Furaha kabisa ktk Nchi Yao, ni hofu na mashaka tele., Tujipange Upya, tuone tunapokosea tuparekebishe haraka, vinginevyo siyo Muda mrefu tunaweza kujikuta tukigawana madirisha na mabati wakati nyumba ni Mali yetu wenyewe