Naingia Shambani very serious kulima Alizeti

Naingia Shambani very serious kulima Alizeti

Mkuu mwakani andaa shamba ekari moja kwenye mbuga isio jaa sana maji au kwenye nkulusi
Kama ni kichanga hakikisha unatumia mbolea ya kukuzia

Lima mapema kabisa mwezi wa 12 uwe umemaliza kulima alizeti

Panda mbegu ya kisasa kwa mstari na vipimo sahihi, ngolea libaki shina moja moja na mawili kwenye vichuguu au shamba lenye rutuba sana.

Palilia kwa wakati na palizi ya maana kama unavyopalilia mahindi( sio kuparaza kama wanavyofanya)

Kama aridhi ni kichanga weka mbolea ya kukuzia baada ya palizi

Vuna mapema usiache alizeti ikauke hadi ianze kupukutika na upepo au wakati wa kuvuna

Omba Mungu wako nvua zinyeshe za kutosha

Utanishukuru baadae

Usilime alizeti mwishoni mwezi wa pili huko
Usipande mbegu za kienyeji wala usipande kienyeji kwa kumwaga mbegu
Usiache mimea imebanana itazaa alizeti kama ngumi
Usianze palizi baada ya mimea kuzongwa na majani itadumaa
Usipalilie juu juu, palilia kama mahindi yanavyotaka
Mkuu samahani kwa huku kwetu morogoro naweza kupanda alizeti hv sasa mwez huu w nne mwanzoni?
 
Mkuu samahani kwa huku kwetu morogoro naweza kupanda alizeti hv sasa mwez huu w nne mwanzoni?
Mkuu sina uzoefu na msimu wa nvua za Morogoro
 
Back
Top Bottom