Naimisi Tanzania ya miaka ya 70

Una maana viwanda vilikufa wakati wa Nyerere au vilikufa watu walipoanza kuvaa mitumba?
Vilikufa wakati wa Nyerere. Viwanda havijaendeshwa kwa faida wala kwa weledi. Ajira na kumsifia Nyerere katika mikutano ya kazini na kuhudhuria mbio za mwenge zilikuwa bora kuliko faida.

Kuna mtu gani mwenye akili timamu na uwezo wa kujikimu maisha anunue mitumba????

Viwanda vya nguo vilikufa. Period.
 
Sasa kama kulikuwa na upungufu wa chakula akaagizia mahindi hata kama ni msaada njaa ilikujaje. Isitoshe Nyerere hakuwa lezi alijua jamaa wanatuwasha na yeye aliwawasha humo kwenye misaada. Kuna mpaka aliyogoma kulipa.
Mwaka 1973-74, kulikuwa na ukame na mafuta yanapanda bei. Pesa za kigeni benki imekauka. Uchumi unaanza kuporomoka pole pole.

Sielewi unataka kunieleza nini hapo. Labda ueleze zaidi serikali ya Marekani ilikuwa inataka kutuwasha vipi?

Unajua hata Urusi, pamoja na vita vya baridi, ilikuwa inanunua mahindi na ngano Marekani. Sababu moja ya Tanzania kutoweza kupata msaada zaidi ni kutokana na u ununuzi mkubwa wa mahindi na Urusi. Nyerere akapewa pesa anunue Malawi na Kenya.

Sent from my SM-G610F using JamiiForums mobile app
 

Tumetoka kwenye facts tumeingia unavyotaka wewe.
 

Sasa si unajinyima chenji mwenyewe hapo. Unamlaumu vipi Nyerere kwa hayo uliyoyasema.
 
Soma hii habari kwa raha zako:

"Arusha — The ogre that swallowed many of the Arusha-based textile factories in the late nineties has returned for another chew onto the remaining two plants, threatening to send these struggling mass employing industrial units into early grave.

A-to-Z and Sun-Flag Textile Mills have so far sent home more than 2,500 workers due to recently emerged cases of cheap, imported bed nets that have started to flood the local market at the expense of the two tax-paying entities of Arusha.

With second-hand garments (mitumba) dictating the country's clothing fashion trends, local fabric manufacturers rely on alternative products such as mosquito nets and bed sheets, the latter command better sales though."
 
naona wewe mwana dar es salaam,mimi nilikuwa kijijini iringa miaka hyo so kitu ambacho na mimi nili enjoy ni hyo radio.......inaumiza kuona wakat wenzetu wakionga mbele sisi tukasonga kwa kuludi nyuma
 
Tulikuwa mpaka na viwanda vya kutengeneza vyandarua. Unakumbuka vibiriti vya Kibo?
 
naona wewe mwana dar es salaam,mimi nilikuwa kijijini iringa miaka hyo so kitu ambacho na mimi nili enjoy ni hyo radio.......inaumiza kuona wakat wenzetu wakionga mbele sisi tukasonga kwa kuludi nyuma

Tumerudi nyuma kisawasawa historia ikitumiwa vizuri inaweza kurekebisha makosa yaliyofanyika. Hata mikoani Dodoma CDA walionyesha mfano bora wa ujenzi wa nyumba za kisasa na zenye ramani. Mijizi na mila rushwa ilipoachiwa tukarudi kwenye ujenzi wa vurugu ambao hata moto ukitokea gari la fire kama likiwepo halitaweza kufika wala huwezi kuita polisi ukawaelekeza jinsi ya kufika nyumbani kwako.
 
Tumetoka kwenye facts tumeingia unavyotaka wewe.
It's a free forum. Sikuzui unachopenda kuandika.

Sijaandika kitu chochote cha uongo na ninachotaka mimi.

Unataka facts zaidi? Korea ya Kusini na Malaysia na Singapore walikuwa na uchumi kama wakati wa uhuru wetu. Leo wametajirika.

Kwa nini unafikiri?

Sent from my SM-G610F using JamiiForums mobile app
 

At least hiyo nukuu hapo juu imekuonyesha viwanda vilikufa lini na kwanini.
 

Hawakuuwa viwanda vyao. Hawakuagiza mitumba na vibiriti waliagiza wawekezaji wa viwanda zaidi.
 
Maisha ya zamani yalikuwa matamu sana
Mie hata sikuona utamu wake.ule wa kupanga foleni duka la kaya au kulimbilia gari la ugawaji.hata sabuni na dawa za meno sigara zilikuwa kuzipata ni mtihani.

Sent from my SM-J700F using JamiiForums mobile app
 
Mie hata sikuona utamu wake.ule wa kupanga foleni duka la kaya au kulimbilia gari la ugawaji.hata sabuni na dawa za meno sigara zilikuwa kuzipata ni mtihani.

Sent from my SM-J700F using JamiiForums mobile app

Duh! rejea mada yote utaona tunazungumzia kipindi cha kabla ya hizo shida. Na pia utajua kwanini hizo shida zilitokea.
 
Sasa si unajinyima chenji mwenyewe hapo. Unamlaumu vipi Nyerere kwa hayo uliyoyasema.
I don't think I can communicate logically with you.

It's very simple. Kama Nyerere angeacha ego yake pembeni na kuruhusu biashara huria, Tanzania ingekuwa na pesa ya kujilipia kila kitu. Ujamaa wake umeua uchumi na kufilisi nchi.

Amini upendavyo. Huwezi hata kwa sekunde moja kunifanya mimi Nyerere apologist.

Believe what you want. It's a free country.

 

Unazungumzia mtu ambaye alijiuzulu akakaa pembeni na kuwaachia nyiye vijana muongoze. Mkaona short cut ni ubinafsishaji kama unavyotaka wewe na kuuwa viwanda kwa kuagizia bidhaa za nje. Unafikiri alishindwa kufanya kama Museveni au Mugabe. Ni ego zipi tena unazozingumzia?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…