Naimisi Tanzania ya miaka ya 70


Toka lini ngano ikanunuliwa kukabili njaa Afrika?
 
Mwaka 74 chapati za maji, chapati za kusukuma, vibibi, maandazi, vitumbua, visheti, mahando, hafu keki, keki, ufuta, bumunda, kashata, kababu, kaimati, mikate ya boflo, mikate ya siha, skonzi, bajia, kachori na vingine ambao watoto waleo hawavijui majina vilikuwa ni chaguo lako. Hakukua na foleni yeyote wala shida yeyote. Wali nyama, pilau, biriani, wali maharage, mseto, ndizi mkono wa tembo, ndizi malindi, pure, (makande) ugali havikuwa na shida.
Wawest Africa mpaka leo wanakula fufu ndio chakula chao. Fufu ni liaina fulani la ugali wa muhogo ambao wabongo hatukuwa na time nao wala hatuna time nao kihivyo.
 
Maisha ya zamani hayakuwa mazuri sana kama tunavyoaminishwa. Nakubali kuwa shuleni nilikuwa hakuna ada au nauli. Lakini shida zilikuwepo nyingi hasa za ukosefu wa chakula. Mara nyingi serikali ilibidi iombe chakula cha msaada. Vijana wa JKT walikosa nguo na hasa viatu. Ilikuwa ni kawaida kuona wamevaa kata mbuga
 

Uwe specific nazungumzia Tanzania kabla ya mwaka 78. Kipindi hiki 77/78 kwenda mbele pia kilihusiana na kuvunjika kwa jumuiya ya afirka mashariki. Tukafungiana mipaka na Kenya. "Manyang'au" waliowahi wakapora mali za Afrika ya mashariki. Katambuga zilitokea kipindi hiki wakenya wakawa na kitendawili ni nchi gani wanavaa matairiiii.
 


Tuko pamoja sasa.
 

Mwaka 1974 kulikuwa na njaa mbaya Tanzania. Hali haikurudi vizuri hadi baada ya vita na njaa nyingine ya miaka ya 80. Mwaka 76 nilikuwa operation mapambano Makutupora. Hakuna hata mmoja aliyepata kiatu. Binafsi nilivaa kata mbuga kwa mwaka mzima. Kila tukilalamika jibu lilikuwa hawana pesa za kuagiza Limuru. Combat pair moja kwa mwaka mzima. Green vest na bukta ilikuwa zinapatikana.
 
Nyinyi ndo wahenga mlobakia inabdi tuwatunze tupate vitu vingi kutoka kwenu

Sent from my TECNO-C5 using JamiiForums mobile app
 
Mwaka 74 tulivaa viatu hivi tulipokwenda shule. Vilitengenezwa na kiwanda cha BATA Kenya. Tena bila ya soksi mstarini asubuhi ilikuwa shida. Unaweza kuchezea fimbo.

 
Na tulivaa kiatu kama hiki. Hiki tulikiita mbwa [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Juu hayo hatukuvaa hivyo viatu wakati tuliposhuka jangwani pale kucheza mpira au tulipocheza mchangani pale Ilala magorofani. Pekupeku ilikubalika hasa wakati wa kuwakimbia wanamgambo uwanja wa Karume tulipokuwa tunaruka ukuta kuingia mpirani bure.
 
Tulikuwa tunakaguliwa usafi wa mwili, nywele na nguo mstarini kila asubuhi.
 
Hapa kuna watu niko nao kama vipofu wanaomshika tembo. Wengine wanashika miguu mimi nashika sikio tutakua na maelezo tofauti. Hiyo Makutopora unayosema mimi darasa la tano nilisoma Dodoma. Nilisoma Dodoma Mlimani nilikaa sehemu inaitwa uzunguni. Tulicheza sana mpira Stoklei pale. Sasa ni njaa ipi unayoizungumzia kipindi hicho.
 

JKT inategemea na utawala kuna kipindi walikumbukwa kuna kipindi walisahauliwa.
 
How soon we forget tulivaa viatu hivi vya BATA kutoka Kenya. Tuliviita maklipa.
 
Toka lini ngano ikanunuliwa kukabili njaa Afrika?
Nimetafsiri vibaya. Nyerere alitaka "corn" / "grain" (mahindi) kutoka Marekani. Hapo chini ni mawasiliano ya Balozi (nimefupisha) wa Marekani alioupeleka Washington, DC:

FIRST, NYERERE SAID HE WANTED TO STRESS TANZANIA'S NEED FOR CORN.

HE HAD HEARD TANGOV HAD REQUESTED 60,000 TONS CORN FROM U.S. TANZANIA'S NEED WAS FOR 100,000 AT MINIMUM BY END FIRST SIX MONTHS 1975.

U.S. HAD AGREED SUPPLY 20,000 TONS FOOD GRAIN UNDER PL 480 TITLE II.

U.S. ALSO IS SUPPLYING ABOUT ONE MILLION DOLLARS FOR SEED CORN TO BE PURCHASED IN MALAWI AND KENYA.

U.S. AGREED TO FORWARD TO WASHINGTON NYERERE'S DEEP PERSONAL WORRY ABOUT FOOD SITUATION FACING TANZANIA AND TO INQUIRE ONCE AGAIN IF THERE IS ANY WAY U.S. COULD HELP TANZANIA OBTAIN CORN BEFORE END FIRST SIX MONTHS 1975.
 
Viwanda vimeongezeka sana. Wakati wa Nyerere viwanda ilikuwa vichache na vyote vya serikali
Na vingi alivitaifisha na kuwaweka watu wasiofahamu biashara. Mwisho wake, vikafa. Ajira na siasa ilikuwa muhimu kuliko faida kazini.



Sent from my SM-G610F using JamiiForums mobile app
 

Sasa kama kulikuwa na upungufu wa chakula akaagizia mahindi hata kama ni msaada njaa ilikujaje. Isitoshe Nyerere hakuwa lezi alijua jamaa wanatuwasha na yeye aliwawasha humo kwenye misaada. Kuna mpaka aliyogoma kulipa.
 
Na vingi alivitaifisha na kuwaweka watu wasiofahamu biashara. Mwisho wake, vikafa. Ajira na siasa ilikuwa muhimu kuliko faida kazini.



Sent from my SM-G610F using JamiiForums mobile app

Una maana viwanda vilikufa wakati wa Nyerere au vilikufa watu walipoanza kuvaa mitumba?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…