Naililia Iramba na umaskini wake!

Mbii mbwane! Ni vizuri umeahidi kufundisha uraia mkoani kwako. But nijuavyo hata mikoa mingine kama Arusha wapinzani wamepata mbunge mmoja ama hamna kabisa. So ni bora hata ya sisi. Kuna mikoa mingine pia CCM hawajapata kitu kama ukienda kule Pemba, nk. Kuna mikoa mingine pia Chadama wameambulia patupu, zaidi hata ya Singida. Ndugu yangu badala ya kumsifia Tundu Lisu ni bora kufanya upembuzi yakinifu. Ninachosisitiza pia sio majimbo kwenda upinzani bali utendajiwa mbunge, awe Chama Tawala ama pinzani. Kuna wabunge Iramba naamini wanaweza wakawa wazuri kuliko hata Tundu Lisu. Kuyaamrisha mashirika ya hiari yaende Singida si hoja bora kwani pia ni kuyadhalilisha mashirika ambayo tayari yapo Singida yakitekeleza ukisemacho. Zaidi nakuhakikishia Tundu Lisu hana tija sana, subiri utaona.

Kukataa chama ni njia ya kwanza kuonyesha kuchoshwa, hata kama wataweka mgombea unayemuona wewe anafaa. Kwani huko monduli na huko singida si walewale tu. Jimbo moja la Arusha mjini limebeba msg kubwa sana ka hujui. Wewe huoni tofauti kati ya jimbo la Arusha mjini na huko kwingine?
 
Naomba sasa tufunge mjadala huu ,majadiliano ya watu kumi na tano yanadhirisha kuwa Iramba inatatizo,tunahitaji kuikomboa bila kujali itikadi zetu.Tuendelee kupambana ! MWASONGELA SANA , KARIBUNI TUUNDE IRAMBA VISION.

Nendeni Kilimanjaro mkajifunze nini maana ya maendeleo. Watu wana maji, umeme, shule za kila namna, barabara za lami na bado wanaendelea kutafuta maendeleo kwa nguvu zote kwa kuchagua viongozi makini, huko kwenu wamebaki kushabikia t-shirt! hatari sana hii
 
hapo sibishi, Maendeleo ya Tanzania Kaskazini yaani mikoa ya Arusha na Moshi yametokana na juhudi ya wananchi wa maeneo hayo na wala si upendeleo wa serikali kama wengi tunavyofikiria.

Sisi tuliotoka mikoa ya kati ambayo wananchi bado wanamelala fofofo ni shughuli kubwa sana kuwaamsha.
a) Watu hawataki mabadiliko
b) Wameridhika na hali ya maisha waliyonayo.
c) Hawana uchu wa maendeleo
d) Hawajui umuhimu wa elimu

Sitaki kuitaja mikoa hii lakini ni ukweli kwamba kuna Makabila mengine kwao maendeleo ni adui, sasa kama mtu kama hataki maendeleo, hataki elimu -- ni kazi kweli kweli.

na mikoa hii ndiyo NGOME YA ccm jiulize why>
 
Sina haja ya kupinga hoja yako, naomba uipinge mwenyewe. Kwa kukudokeza tu kuna factors nying sana kuhusu hali hiyo katika mikoa hiyo. Si kama unavyofikiri
 
Nendeni Kilimanjaro mkajifunze nini maana ya maendeleo. Watu wana maji, umeme, shule za kila namna, barabara za lami na bado wanaendelea kutafuta maendeleo kwa nguvu zote kwa kuchagua viongozi makini, huko kwenu wamebaki kushabikia t-shirt! hatari sana hii
Kukubali Changamoto na kukubali Tatizo ni mwanzo mzuri wa kutatua tatizo.
Nakubaliana nawe PAX kuhusu kilimanjaro na hili linatokana na watu kupenda eneo lao na kutokuwa wanafiki, watu wa singida nami nikiwemo ni wabinafsi na wanafiki, hawapendi asili yao na pia si wakweli, mtu anapowadanganya badala ya kusema ni muongo wanazunguka mbuyu. wamejaa unafiki na ufitina na kamwe kwa tabia hii singida haitaendelea. WITO wana singida tubadilike tupende tulikotoka na tuamua kwa dhati kupinga adui wa kwanza wa umasikini wetu Uongozi. sikubaliani kabisa na falsafa kwamba kwa kuwa dewji anatoa misaada basi ni kiongozi mzuri hat kidogo. singida ina rasilmali nyingi na zikipata vichwa vizuri zinaweza badilisha maisha ya wana singida na sio kutegemea vipipi tunavyolishwa na viongozi uchwala kama Dewji na wenzake
 
Antua aane swee......!
Kushoke kukaa.....ishe sika kukushoka..... Anga kusamile ku-mujini kwi yiwa pena kaa.......! Kuleki gona kuuke...! Tyunu mau inye....!
 
Back
Top Bottom