Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 23,282
- 33,880
Montaza Palace, Alexandria June 1988
View attachment 1013504
Ndugu zangu nilikuwa napita Maktaba Idara ya Picha.
Nia yangu ni kuandika kitu kidogo kuhusu mji wa Alexandria.
Katika pekua pekua nikakuta picha hiyo hapo juu niliyopiga Port Said Holiday Hotel.
Ilikuwa Jumatano Juni 15, 1988.
Hii picha yangu ikanishtua kidogo na kilichonishtusha ni mkao wangu.
Nakuombeni muweke "caption," ya picha hii.
Alexandria ni katika miji mizuri duniani na sishi kuukumbuka lakini kwa sasa nitaukumbuka zaidi pamoja na magoli 5 waliyofungwa Simba na Al Ahly.
Ijumaa moja niliswali sala ya Ijumaa Montaza Palace, Alexandria.
Hii ilikuwa kasri la Kiangazi la King Farouk na baada ya mapinduzi ya Gamal Abdel Nasser 1952 Montaza Palace ikawa moja ya majumba ya fahari ya serikali.
Ndani ya Montaza Palace kuna msikiti mzuri sana ambao niliswali Ijumaa nikifuatana na mwalimu wanvu mmoja kutoka Arab Maritime Transport Academy (AMTA) chuo kikubwa Arabuni yote katika mambo ya bahari.
Baada ya sala mwalimu wangu huyu akaniuliza kama nimeweza kuelewa khutba ambayo ilikuwa ya Kiarabu.
Alishangaa nilipomwambia kuwa khutba ilikuwa kuhusu hijja.
Nikamwambia nimeelewa khutba ile kutokana na aya za Qur'an kuhusu Hijja.
Mwalimu wangu yule akaniuluza iweje nielewe Qur'an lakini sijui lugha ya Kiarabu?
Hii Montaza Palace ina sehemu muhimu moyoni kwangu kutokana kitabu cha Mohamed Hasnain Heykal, "The Road to Ramadan," alichoandika kuhusu Vita Vya Yom Kippur baina ya Misri, Syria na Israel mwaka wa 1973.
Baada ya mafanikio makubwa katika uwanja wa mapambano Anwar Sadat alikwenda Montaza Palace huku vita vikiendelea.
Heykal mwandishi mkubwa sana aliyekuwa mhariri wa gazeti la Alahram la Misri alikwenda Montaza Palace kufanya mahojiano na Sadat.
Heykal katika staili yake ya uandishi wa "satire," kwa jambo asilopenda kwenye kitabu hicho anasema kamkuta Sadat ana glasi ya kinywaji.
Akampa swali.
Sadat hakujibu akaongeza kinywaji kwanza.
Taratibu akawa anakunywa hadi akamaliza ndipo akafungua kinywa chake akasema, "Mohamed mimi ni Amiri Jeshi Mkuu hayo maswali yako wapelekee wanasiasa Cairo watakujibu."
Katika sura hii Heykal anamnanga sana Sadat anasema uniform yake ya Commander in Chief aliagizisha kwa ‘’designer,’’ mabingwa wa mitindo ya nguo kampuni maarufu ya Paris - Yve Saint Laurent.
Kuna mengi ya kejeli Heykal kaandika...kila ninapoikumbuka Alexandria nakumbuka Montaza Palace, Sadat, Heykal...na goli 5.
salaam,Montaza Palace, Alexandria June 1988
View attachment 1013504
Ndugu zangu nilikuwa napita Maktaba Idara ya Picha.
Nia yangu ni kuandika kitu kidogo kuhusu mji wa Alexandria.
Katika pekua pekua nikakuta picha hiyo hapo juu niliyopiga Port Said Holiday Hotel.
Ilikuwa Jumatano Juni 15, 1988.
Hii picha yangu ikanishtua kidogo na kilichonishtusha ni mkao wangu. Nakuombeni muweke "caption," ya picha hii.
Alexandria ni katika miji mizuri duniani na sishi kuukumbuka lakini kwa sasa nitaukumbuka zaidi pamoja na magoli 5 waliyofungwa Simba na Al Ahly.
Ijumaa moja niliswali sala ya Ijumaa Montaza Palace, Alexandria. Hii ilikuwa kasri la Kiangazi la King Farouk na baada ya mapinduzi ya Gamal Abdel Nasser 1952 Montaza Palace ikawa moja ya majumba ya fahari ya serikali.
Ndani ya Montaza Palace kuna msikiti mzuri sana ambao niliswali Ijumaa nikifuatana na mwalimu wanvu mmoja kutoka Arab Maritime Transport Academy (AMTA) chuo kikubwa Arabuni yote katika mambo ya bahari.
Baada ya sala mwalimu wangu huyu akaniuliza kama nimeweza kuelewa khutba ambayo ilikuwa ya Kiarabu. Alishangaa nilipomwambia kuwa khutba ilikuwa kuhusu hijja. Nikamwambia nimeelewa khutba ile kutokana na aya za Qur'an kuhusu Hijja. Mwalimu wangu yule akaniuluza iweje nielewa Qur'an lakini sijui lugha ya Kiarabu?
Hii Montaza Palace ina sehemu muhimu moyoni kwangu kutokana kitabu cha Mohamed Hasnain Heykal, "The Road to Ramadan," alichoandika kuhusu Vita Vya Yom Kippur baina ya Misri, Syria na Israel mwaka wa 1973.
Baada ya mafanikio makubwa katika uwanja wa mapambano Anwar Sadat alikwenda Montaza Palace huku vita vikiendelea.
Heykal mwandishi mkubwa sana aliyekuwa mhariri wa gazeti la Alhram la Misri alikwenda Montaza Palace kufanya mahojiano na Sadat. Heykal katika staili yake ya uandishi wa "satire," kwa jambo asilopenda kwenye kitabu hicho anasema kamkuta Sadat ana glasi ya kinywaji.
Akampa swali.
Sadat hakujibu akaongeza kinywaji kwanza.
Taratibu akawa anakunywa hadi akamaliza ndipo akafungua kinywa chake akasema, "Mohamed mimi ni Amiri Jeshi Mkuu hayo maswali yako wapelekee wanasiasa Cairo watakujibu."
Katika sura hii Heykal anamnanga sana Sadat anasema uniform yake ya Commander in Chief aliagizisha kwa ‘’designer,’’ mabingwa wa mitindo ya nguo kampuni maarufu ya Paris - Yve Saint Laurent.
Kuna mengi ya kejeli Heykal kaandika...kila ninapoikumbuka Alexandria nakumbuka Montaza Palace, Sadat, Heykal...na goli 5.
Msaga Sumu,salaam,
mzee wangu unamaanisha nini unapsema baada ya Sadaat kupata ushindi mkubwa kwenye uwanja wa vita? pia Misri iliwahi kutoa watu wawili watata sana ndg Ayman Zawahiri na bwana Sayyid Qutb bila shaka unawafahamu hawa
Kawombe,Hatar sana hakika ulifaidi sana
Sent from my iPhone using JamiiForums
sMsaga Sumu,
Maana yangu ni kuwa vita vilikuwa vinawaendea vyema.
Hao ni maarufu ila kwangu mimi mtu mtata kutoka Misri ni
Osama Al Baz.
shukran sana,huyu Osama simjui ila acha nimtafute ni msome nae,hao wawili nilikutana nao kwenye kitabu fulani nikavutiwa nao sanaMsaga Sumu,
Maana yangu ni kuwa vita vilikuwa vinawaendea vyema.
Hao ni maarufu ila kwangu mimi mtu mtata kutoka Misri ni
Osama Al Baz.
Kawombe,
Kusafiri ni kuzuri sana.
Offshore...Mzee shikamoo, nashukuru kwa kutupa historia nzuri.
Samahani Ulipita katika chuo cha Arab Maritime Transport Academy (AMTA) kwa masuala ya kitaaluma.
Sent using Jamii Forums mobile app
Mzee wangu tunaomba uandike vitabu ili utuachie zawadi ya kipaji na historia unayoifahamu.
Kupitia vitabu itakuwa ni zawadi kwa vizazi na vizazi pia mchango wako hautofutika kwa jamii yetu.
Sent using Jamii Forums mobile app
Sky...Shukran mzee, pia Epypt Air hutoa mar ubani wenye uzoefu wa kurusha ndege. Ukitaka kujua uzoefu wa rubani ni pale ndege inapotua husikii ile hali ya disgust kutembea tumboni mpaka kukukera.
Janguo era.Sky...
Umezungumza kuhusu ndege - Egypt Air.
Nimepanda Egypt Air mara tatu.
Dar - Cairo - Dar.
Dar - Cairo - London - Dar
Dar - Cairo - Berlin - Dar
Asante sana mzee wangu.Offshore...
Naam kulikuwa na program ya UNCTAD inaitwa Improved Port Perfomance (IPP) ilitengenezwa Chuo Kikuu Cha Cardiff, Wales ikawa inasomeshwa dunia nzima. Nilihudhuria mafunzo hayo na wanafunzi wengine kutoka Frontline States pamoja na Nigeria na Kenya na vyama vya ukombozi ANC, FRELIMO na wengineo. Walifadhili serikali ya Misri. Nitakuwekea picha In Shaa Allah.
View attachment 1013792
Ismailia, Misri Juni 1988
Sent using Jamii Forums mobile app