Wadau. Hii spika wakati nainunua nilijua kabisa ni mbovu ila nikajipa moyo huenda itatengenezeka. Lakini wapi.
Chaajabu imezidi kuwa ya hovyo hovyo kadiri muda unavyoenda. Kila mara naitibia maradhi yake inapona kidogo halafu inaanza tena kusumbua. Imefikia hatua mpaka naficha gharama za kuitibu maana mtahisi labda nawafanyieni ufisadi. Gharama ni kubwa mno unafikiri nanunua music system nzima kumbe NI utengenezaji tu wa spika moja mbovu.
Hii spika bhana nimeshindwa kuielewa. Imeanza kuingilia hadi kazi ya calculator - kile kikokotoa hesabu. Yaani imekuwa ya hovyo Sana.
Kwakweli Mimi binafsi naona hainifai Tena. Kuna wakati kijispika kidogo Cha pembeni kilipigwa short za moto zaidi ya Mara 20, cha ajabu hii spika yangu kubwa badala ya kuendelea kuimba vizuri ili itoe sapoti kwaile ya pembeni ndio kwanza ikaanza kukoroma na kuzima kabisa.
Yaani hapa nimechukia Sana. Ilivyo ya ajabu Mimi nikitaka ipige mziki huu yenyewe inacheza mziki mwingine tofauti kabsaa. Jana nimekasirika Sana ilipoanza kucheza mziki wa Afrika kusini Tena kukandamiza kajispika ambako NI kabrand moja na yeye. Vitu vya ajabu Sana.
Jamani nisiwachoshe. Naigawa bure. Kwa Sasa Sina KAZI nayo kabisa. Spika haijielewi. Inanitia gharama za bure tuu. Mwenye kuihitaji hii nimeiweka njiani tuu hapo makao mapya
Wasaalaam