Naigawa spika yangu bure kabisa

TAI DUME

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2014
Posts
11,487
Reaction score
31,672
Wadau. Hii spika wakati nainunua nilijua kabisa ni mbovu ila nikajipa moyo huenda itatengenezeka. Lakini wapi.
Chaajabu imezidi kuwa ya hovyo hovyo kadiri muda unavyoenda. Kila mara naitibia maradhi yake inapona kidogo halafu inaanza tena kusumbua. Imefikia hatua mpaka naficha gharama za kuitibu maana mtahisi labda nawafanyieni ufisadi. Gharama ni kubwa mno unafikiri nanunua music system nzima kumbe NI utengenezaji tu wa spika moja mbovu.
Hii spika bhana nimeshindwa kuielewa. Imeanza kuingilia hadi kazi ya calculator - kile kikokotoa hesabu. Yaani imekuwa ya hovyo Sana.

Kwakweli Mimi binafsi naona hainifai Tena. Kuna wakati kijispika kidogo Cha pembeni kilipigwa short za moto zaidi ya Mara 20, cha ajabu hii spika yangu kubwa badala ya kuendelea kuimba vizuri ili itoe sapoti kwaile ya pembeni ndio kwanza ikaanza kukoroma na kuzima kabisa.

Yaani hapa nimechukia Sana. Ilivyo ya ajabu Mimi nikitaka ipige mziki huu yenyewe inacheza mziki mwingine tofauti kabsaa. Jana nimekasirika Sana ilipoanza kucheza mziki wa Afrika kusini Tena kukandamiza kajispika ambako NI kabrand moja na yeye. Vitu vya ajabu Sana.

Jamani nisiwachoshe. Naigawa bure. Kwa Sasa Sina KAZI nayo kabisa. Spika haijielewi. Inanitia gharama za bure tuu. Mwenye kuihitaji hii nimeiweka njiani tuu hapo makao mapya

Wasaalaam
 
Ni bora ukaiuza hata kwa hasara tu ili ufidie gharama zako za manunuzi. Na kwa sasa hiyo spika unayo hapo "jijini" Dodoma au umeiacha kule nyumbani Kongwa?
 
Hii spika ndugu yangu itakuletea tabu tu huko mbeleni, ni bora ungeshtuka mapema sana kabla haijakuaibisha zaidi mbele ya wageni

Kama wewe umeitegesha iliye mziki huu halafu inarukia mziki mwingine huoni kuna aibu kubwa huko mbeleni?

Tena nakushauri usiigawe wala usiipeleke kwenye matengenezo tena, ITUPE STORE TU ILI UTAFUTE NYINGINE.
 
Kuna jamaa yangu yuko Uganda anahitaji nikuunganishe naye! Yeye anasema vilivyokufa ndo vinamfaa
 
Bado tuna washairi bora kiasi hiki

Hili ni shairi bora Kabisa

Tafadhali mhusika weka beti , mezani na vina

Hakika ukishindanishwa huna mpinzani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…