tonicimmobility
JF-Expert Member
- Jun 17, 2025
- 493
- 1,038
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Wanu Hafidh Ameir, amevitaka vyuo vya Ufundi Stadi (VETA) nchini kurejesha kozi za muda mfupi za kilimo na ufugaji zilizokuwa zimesitishwa, ili kuwawezesha Vijana kupata ujuzi unaoendana na mahitaji ya maeneo yao na kujiajiri baada ya kuhitimu.
Wanu ametoa maelekezo hayo leo, Novemba 26, 2025, wakati wa ziara yake katika Chuo cha VETA Chemba, ambapo pia alizindua ugawaji wa vifaa vya mafunzo kwa Vyuo 63 vya VETA nchini kwa Kanda ya Kati.
Amesema VETA ni taasisi muhimu na ya kimkakati katika kuchangia utekelezaji wa ajenda ya maendeleo ya nchi, hususan katika kukuza uchumi kulingana na Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, huku akivielekeza vyuo hivyo kujikita katika kutoa mafunzo yanayochochea matumizi ya TEHAMA, ikiwemo Akili Mnemba (AI) na teknolojia ya roboti, ili kuendana na mahitaji ya Uchumi wa Kidijitali.
Wanu amesema Tanzania inaendelea kupiga hatua katika Sekta ya Viwanda na Uchumi, huku maeneo ya uwekezaji yakiongezeka kufuatia ujenzi wa viwanda vikubwa na vya kati. Amesisitiza kuwa mafanikio hayo yanahitaji nguvu kazi yenye ujuzi na maarifa ya kutosha.
Aidha, amesema kuwa serikali imejipanga kuhakikisha VETA inapatiwa vifaa vya kisasa kwa ajili ya mafunzo, na kuiagiza taasisi hiyo kuzingatia ubora wa utoaji wa elimu ili uendane na mahitaji ya soko la ajira ndani na nje ya nchi.