real G
JF-Expert Member
- Feb 7, 2013
- 5,227
- 5,292
Naibu waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ( TAMISEMI) Suleman Jafo amewataka wakuu wa wilaya zote nchi kutoburuzwa na wakurugenzi pamoja na baadhi ya watendaji katika kusimamia fedha za miradi ya serikali huku akiwataka wakurugenzi wa Halmashauri kuacha ubinafsi na badala yake wawashirikishe wakuu wa wilaya katika mipango yote ya maendeleo.