Naibu Waziri wa Nishati na Madini: Uranium kama malighafi haina madhara ya mionzi!

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
11,143
18,774
Nadhani ni mara ya pili nasikia kiongozi wa juu wa Taifa akisema kuchimba madini ta uranium hakuna madhara ya mionzi, akitoa wazo kwamba uranium kama malighafi haina madhara hadi itakapokuwa "processed".

Nadhani huu ni ukihiyo, na viongozi wetu hawapaswi kutoa kauli zenye kupotosha kama hizi, ukizingatia kwamba mwananchi wa kawaida atadhani uranium ikitolewa ardhini haina madhara hadi itakapokuwa processed.

Angalia alichosema Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Stephen Masele;

Naibu Waziri huyo alisema kazi ya Wizara ya Nishati na Madini ni kutoa leseni baada ya Nemc kufanya tathmini ya athari ya kimazingira. Hata hivyo, alisema kinachotarajiwa kuchimbwa nchini ni malighafi, ambayo kwenye ardhi ya Tanzania ipo na haijaleta madhara yoyote.

Source: IPP Media
 
Naibu Waziri, wacha kupotosha Watanzania. Uranium faida yake ni ndogo, lakini madhara
yake ni ya milele. Serikali binafsi haijachunguza faida na madhara ya Uranium, na bado
amjawaelimisha wananchi juu ya madhara ya Uranium, kwa sababu wakulima wa eneo ilo
wasingetumia uranium kumwagia mashambani kama dawa ya kuua wadudu. Je watumiaji
wa chakula hicho watakuwa salama.
 
Back
Top Bottom