Naibu Waziri wa nchi mazingira na muungano awazawadia washindi wa tamasha la ajira na ujasiriamali

RAHA KAMILI

JF-Expert Member
Dec 5, 2014
203
83
IMG_5189.JPG


Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano Mh Luhanga Mpina akikabidhi zawadi kwa washindi wajiojishindia zawadi mbalimbali kutoka kampuni ya huawei kwenye tamasha la ajira na ujasiriamali lililofanyika Chuo kikuu Mzumbe Mkoani Mbeya.

Chuo kikuu cha Mzumbe jijini Mbeya kiliendesha kongamano la Ujasiliamali ambalo lilihuishwa na shindano la “badirika kwa vitendo” ambapo wanafunzi sita walijishindia zawadi mbalimbali zikiwemo simu za mikononi toka kampuni ya Huawei.

IMG_5211%2B%25281%2529.JPG


Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano Mh Luhanga Mpina katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji Clouds Media Group Ruge Mutahaba na Afisa Mtendaji Mkuu wa EAG group Imani Kajula na washindi waliojinyakulia zawadi mbalimbali.
IMG_5161.JPG
Mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji Clouds Media Group Ruge Mutahaba ambaye naye alitoa mada mbalimbali namna ya kukabiliana na changamoto ya ajira hapa nchini
IMG_5145.JPG
Afisa Mtendaji Mkuu waEAG group Imani Kajula akitoa mada kwenye tamasha la ajira na ujasiriamali lililofanyika mkoani Mbeya

Katika hafla hiyo ya usiku, wanafunzi hao sita Elisha Tullo, Nelson Mkolozi, Goodlove Msigwa, Agness Ngusa, Leornard Meshack walieleza walichojifunza na jinsi watakavyotumia ujuzi wao. Mshindi wa kwanza alikuwa ni Elisha Tullo na wa pili alikuwa Goodlove Msigwa.

IMG_5122.JPG


IMG_5123.JPG




IMG_5154.JPG


Washiriki wa tamasha hilo wakisikiliza kwa makini mda mbalimbali zilizowasilishwa kwenye tamasha la ajira na ujasiriamali lililofanyika chuo kikuu Mzumbe kampasi ya Mbeya kuona picha zaidi za washindi na usiku wa wajasiliamali
 
Back
Top Bottom