Naibu Waziri wa mambo ya ndani awaonya wakimbizi

Gama

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
13,265
4,729
pic+wakimbizi.jpg

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni ametoa onyo hilo leo wakati akiwahutubia wananchi hao wanaoishi kwenye makazi ya wakimbizi ya Katumba, kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Nduwa.

Sumbawanga. Serikali imewaonya na kuwatahadharisha raia wake wapya ambao awali walikuwa wakimbizi wanaoishi katika makazi ya Katumba wilayani Mpanda mkoani Katavi kuwa itawachukulia hatua za kisheria wale wote ambao wanaingiza silaha na kufanya vitendo vya ujambazi na ujangili.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni ametoa onyo hilo leo wakati akiwahutubia wananchi hao wanaoishi kwenye makazi ya wakimbizi ya Katumba, kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Nduwa.
Amesema Serikali kupitia vyombo vyake vya ulinzi na usalama, haitasita kuwachukulia hatua kali za kisheria wale wote watakaobainika kufanya hivyo kwani kupewa uraia wa hapa nchini sio sababu ya wao kufanya vitendo uhalifu na ujangili unaotishia kumaliza rasilimali zetu.
Masauni amesema taarifa zilizopo zinaonyesha kwamba baadhi raia hao wapya waliopewa uraia miaka ya karibuni wamekuwa sio waaminifu na vinara wa vitendo vya uhalifu hususani ujangili na ujambazi wa kutumia silaha za moto.

Chanzo: Mwananchi
 
Back
Top Bottom