Serikali Kuanza Mahojiano Rasmi na Wakimbizi - Naibu Waziri Daniel Sillo

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
2,756
1,261

SERIKALI KUANZA MAHOJIANO RASMI NA WAKIMBIZI - NAIBU WAZIRI DANIEL SILLO

Serikali ya Tanzania inatarajia kuanza mahojiano ya kina na wakimbizi wa Burundi wanaoishi nchini ifikapo 2025. Mahojiano yatashirikisha wadau mbalimbali, ikiwemo Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Wakimbizi (UNHCR).

Lengo kuu ni kubaini changamoto wanazokabiliana nazo wakimbizi na kutafuta suluhisho la kudumu kulingana na maoni yatakayokusanywa katika mahojiano.

Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Daniel Sillo, alipowasilisha ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa 75 wa Kamati Tendaji ya UNHCR nchini Uswisi, tarehe 15 Oktoba 2024.

Mhe. Daniel Sillo alibainisha kwamba Tanzania inahifadhi wakimbizi zaidi ya 240,000, wengi wao wakiwa kutoka Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Alisema Serikali imefanikiwa kutafuta suluhisho la kudumu kwa wakimbizi 17,283 kwa mwaka huu, ambapo wakimbizi 12,717 walirudi kwa hiari katika nchi zao za asili na 4,566 walipatiwa makazi mapya katika mataifa mengine.

Aidha, Mhe. Daniel Sillo katika Ujumbe wake alieleza kuwa licha ya Mafanikio hayo, Operesheni za Kuhudumia Wakimbizi nchini Tanzania inakabiliwa na changamoto kubwa za kifedha, hasa katika sekta za afya na elimu katika kutoa huduma bora kwa Wakimbizi

Kwa upande wake, Kamishna Mkuu wa UNHCR, Filippo Grandi ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa juhudi zake katika kuhifadhi wakimbizi kwa miaka mingi na sasa kujikitika katika kutafuta suluhisho la kudumu kwa Wakimbizi hao. Aidha alitoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuungana ili kusaidia wahanga wa migogoro na kuhakikisha wanapata misaada inayohitajika

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Daniel Sillo, pamoja na mwenyeji wake, Balozi Hoyce Temu Naibu Mwakilishi wa kudumu Uswisi, na Mkurugenzi wa Idara ya Huduma kwa Wakimbizi Tanzania, Sudi Mwakibasi, wameshiriki ufunguzi wa mkutano wa 75 wa Kamati Tendaji ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR). Mkutano huo umefanyika, Oktoba 14, 2024, katika mji wa Geneva nchini Uswisi.

Mkutano huu unalenga kuimarisha ushirikiano wa Kimataifa katika kukabiliana na ongezeko la Wakimbizi, sambamba na kujadili changamoto mbalimbali zinazowakabili Wakimbizi duniani.
 

Attachments

  • GZ_96AMWwAAwGjW.jpg
    GZ_96AMWwAAwGjW.jpg
    99.5 KB · Views: 4
  • GZ7U3PTWEAAMQwi.jpg
    GZ7U3PTWEAAMQwi.jpg
    79.2 KB · Views: 3
  • GZ7CuUEXoAA4H_b.jpg
    GZ7CuUEXoAA4H_b.jpg
    99.1 KB · Views: 4
  • GZ7CXvtWMAADVSE.jpg
    GZ7CXvtWMAADVSE.jpg
    81.3 KB · Views: 4
  • GZ7CXv0XoAA7Zv_.jpg
    GZ7CXv0XoAA7Zv_.jpg
    101.2 KB · Views: 4
  • Screenshot 2024-10-16 at 15-19-03 Wizara_Mambo ya Ndani ya Nchi (@wizaramnn) • Instagram photo...png
    Screenshot 2024-10-16 at 15-19-03 Wizara_Mambo ya Ndani ya Nchi (@wizaramnn) • Instagram photo...png
    675.8 KB · Views: 4
  • Screenshot 2024-10-16 at 15-18-12 Wizara_Mambo ya Ndani ya Nchi (@wizaramnn) • Instagram photo...png
    Screenshot 2024-10-16 at 15-18-12 Wizara_Mambo ya Ndani ya Nchi (@wizaramnn) • Instagram photo...png
    610.2 KB · Views: 3
  • Screenshot 2024-10-16 at 15-18-36 Wizara_Mambo ya Ndani ya Nchi (@wizaramnn) • Instagram photo...png
    Screenshot 2024-10-16 at 15-18-36 Wizara_Mambo ya Ndani ya Nchi (@wizaramnn) • Instagram photo...png
    791.5 KB · Views: 4
Back
Top Bottom