Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Ridhiwan Kikwete awabana wakuu wa idara

Elitwege

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
5,154
10,809
Chalinze. Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Ridhiwan Kikwete amewainua baadhi ya wakuu wa idara aliokuwa ameambatana nao kwenye ziara yeke kujibu kero zilizotolewa na wananchi wa vijiji vitatu katika kata ya Miono Halamashauri ya Chalinze mkoani Pwani.

Ridhiwan ambaye alikuwa kwenye ziara na kufanya mikutano ya hadhara katika vijiji vitatu vya kata ya Miono amesema wakuu wa idara ndio wanatakiwa kujibu kero zinazotolewa na wananchi.

Katika mikutano yake ya hadhara, baadhi ya wananchi waliwasilisha changamoto zinazowakabili huku wakimuomba azitolee majibu.

Baadhi ya changamoto zilizotajwa wakati wa mikutano hiyo ni zinazohusu ardhi, elimu na afya ambapo wananchi hao wamelalamikia huduma mbovu katika baadhi ya vituo vya afya na zahanati ikiamo ukosefu wa chanjo kwa watoto wachanga pamoja na migogoro ya ardhi.

Wananchi hao wameibua kero hizo kwenye mikutano ya hadhara iliyofanyika katika vijiji vitatu vya Kwaikonje, Masimbani na Miono vilivyopo kata ya Miono wakati wa ziara ya Naibu Waziri huyo.

Baada ya wananchi kuwasilisha kero hizo, Ridhiwani ambaye ni Mbunge wa Chalinze alianza kuwaita wakuu wa baadhi ya idara alioambatana nao na kuwataka watoe majibu kwa wananchi.

Amesema wananchi wanachotaka ni kuona maendeleo na sio kila wakati kuahidiwa ndio maana katika ziara hiyo ameambatana na wataalamu mbalimbali wakiwemo wa Ardhi, Afya, Elimu, Barabara na Nishati ambapo aliwawainua mmoja baada ya mwingine kutoa majibu ya kero hizo ambapo amesema hataki awe msemaji huku wahusika wa moja kwa moja wakiwepo.

"Lazima na sisi Chalinze tutamani watoto wetu wafanikiwe kama walivyofanikiwa wenzetu kwa hiyo nashauri kila mtu atimize wajibu wake "amesema Ridhiwan.

Wakitoa majibu ya kero hizo, Kamishna wa Ardhi Mkoa wa Pwani, Lucy Kabemela amesema migogoro mingi ya ardhi inatokana na watu kutosimamia sheria zilizopo.

Kwa upande wake kaimu Ofisa Elimu Chalinze, Iren Lubega amesema tatizo la elimu linachangiwa na wazazi kutokuwa na mwamko ambapo baadhi wanawakataza watoto kufanya vizuri katika mitihani yao huku akiwataka wazazi kuacha tabia hiyo.

Advertisement

Kuhusu uhaba wa chanjo kwa watoto, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chalinze, Msongo Songoro ameeleza kuwa imetokana na baadhi ya zahanati kukosa majokofu ya kuhifadhia dawa hizo na kwamba katika bajeti ijao watalifanyia kazi.

Awali akiwasilisha kero hizo, Diwani kata ya Miono, Juma Mpwimbwi amesema baadhi ya wazazi wamekuwa wakiwakataza wanafunzi kufanya vizuri darasani ili wasifaulu kwa sababu hawana fedha za kuendelea kuwahudumia sekondari.

"Leo nasema ukweli japo utauma hapa watoto wana uwezo mzuri tu darasani kasheshe iliyopo wazazi wengi hawataki wafaulu wanawaambia kabisa wasifanye vizuri mitihan eti hawana hela ya sekondari si uongo huu, elimu sasa ni bure na kama bweni gharama ni ndogo waache visingizio tutafungana na usiingilie tafadhali "amesema Mpwimbwi

Mkazi wa kijiji cha Kwaikonje, Mwamini Nyangasi amesema migogoro ya mipaka ikiwemo ya kijiji cha Kwaikonje na Mbwewe inarudisha nyuma maendeleo.

Kwa upande wake Khatibu Mhina ambaye ni mkazi wa Masimbani amedai kuwa katika zahanati ya eneo hilo hakuna chanjo ya watoto wachanga na wanalazimika kuifata mbali ambapo ni gharama.

"Pamoja na kero zilizowasilishwa tayari, tunaomba ujue tuna shida ya jengo la wajawazito Miono, chumba kilichopo kidogo mno, hakuna dawa mara nyingi tunaambiwa tukanunue"
 
Huyu ni miongoni mwa Maraisi wanao andaliwa kuongoza nchi hi baada ya Mama kumaliza mihula yake, January Nape au Ridhiwani moja wao atakua mwenye kiti wa chama.......kubali au kataa hizo ndo siasa za nchi zetu za Africa

Shindwa shindwa shindwa
 
😳 ninani naibu? aisee ule umwinyi wa zenji nauona tanganyika
 
Utakubali hi Tz sio ya bibi yako inawenyewe huna la kufanya masikini duh
Na huo ndio ukweli watu wakubali wakatae huyu dogo anaandaliwa kuwa rais wa jamhuri ya muungano wa tanzania
 
Huyu ni miongoni mwa Maraisi wanao andaliwa kuongoza nchi hi baada ya Mama kumaliza mihula yake, January Nape au Ridhiwani moja wao atakua mwenye kiti wa chama.......kubali au kataa hizo ndo siasa za nchi zetu za Africa
Ndio ukweli huo halafu watu hawajui tu kuwa nchi hii wenye maamuzi ni watu wachache sana
 
Ndio ukweli huo halafu watu hawajui tu kuwa nchi hii wenye maamuzi ni watu wachache sana
Wa kiambiwa katiba mpya ni muhimu wanafikiri Mbawe anatafuta umaarufu wa kisiasa sasa hayo ndo mtokeo kumpa mtu moja mamalaka mengi kuliko raia wenyewe.
 
Huyu ni miongoni mwa Maraisi wanao andaliwa kuongoza nchi hi baada ya Mama kumaliza mihula yake, January Nape au Ridhiwani moja wao atakua mwenye kiti wa chama.......kubali au kataa hizo ndo siasa za nchi zetu za Africa
Pamoja nawewe wote wahuni na wapigaji Ndio kuendelea kuididimiza Tanzania.
Hawafai kabisa hawa kwanza wameshajilimbikiza mali sana.
 
Back
Top Bottom