Naibu waziri wa Afya Hadmis Kigwangallah aibukia hospitali ya Temeke

magode

JF-Expert Member
Oct 2, 2014
2,204
3,337
Wanabodi
Salaam;

Ule mwendelezo wa safari za kushtukiza umeendelea tena leo kwa naibu waziri kutembelea hosp.ya rufaa ya temeke kwa kushtukiza jioni hii..

Kuna taarifa ambazo me sijazithibitisha akiwa pale amewasimamisha kazi manesi 4 ambao inadaiwa walichukuwa pesa za wagonjwa kwa maelezo ya kununulia vifaa vya kujifungulia. Mwenye taarifa kamili atuwekee hapa.

Me nimeshuhudia nikiwa nje na nilishindwa kupiga hata picha kutokana na kutingwa na majikumu yangu..lkn wanahabari wengi walikuwepo..

Nawasilisha.
 
Mwenyezi Mungu awajalie hekima,Busara na utendaji wa haki ktk utekelezaji wa majukumu yao waheshimiwa wabunge na mawaziri..msirudi nyuma,fanyeni kazi kwa kuendelea kujituma,moyo thabiti,ukakamavu kiufahamu...Tanzania mpya imekaribia nayo ipo karibu...
 
Hii Mbona ilikuwa kwenye taarifa ya habari ya saa mbili ITV. Ni kweli kuna wauguzi wamesimamishwa kazi kwa tuhuma za Rushwa na ubadhilifu, moja wapo ikiwa ni kuwauzia kina mama wajawazito mipira ya mikononi (Gloves) kwa shilingi 5000/= ...ilhali hapo nje famasi mipira hiyo hiyo inauzwa shilingi 1000/=.

Wauguzi pia wanatuhumiwa kwa kukataa kutoa huduma za matibabu kwa wagonjwa wanaootumia Bima ya Afya kwa kuwa haina maslahi kwao. Mwananchi mmoja aliyekuwa na mgonjwa wake alihoji juu ya suala la Bima kuna Muuguzi akamjibu kwa kejeli "HAPA NI CHANGANYIKENI MJIPANGE".
Nafikiri imefikia wakati hawa Wauguzi wanatakiwa kupewa Elimu juu ya Huduma kwa Wagonjwa.
Chanzo : ITV HABARI.
 
Hizo ngonjera mwisho mwisho watu watazizoea na itakuwa kama juzi na jana tu. Kwa taarifa yenu Nyerere alikuwa mwadilifu na mkali kuliko Pombe lakini alibwaga manyanga. Achana na Tz bana. Hii kitu ni sugu eti.
 
Hizo ngonjera mwisho mwisho watu watazizoea na itakuwa kama juzi na jana tu. Kwa taarifa yenu Nyerere alikuwa mwadilifu na mkali kuliko Pombe lakini alibwaga manyanga. Achana na Tz bana. Hii kitu ni sugu eti.
Nyetik mkubwa weeee....
 
Back
Top Bottom