Naibu waziri Mwita Waitara amekurupuka!

Tulimumu

JF-Expert Member
Mar 11, 2013
14,305
12,968
HII NCHI INA VITUKO VYAKE
Nimesikia Tamko la naibu waziri Tamisemi kuwa hata kama Mzazi hajalipa Ada katika Shule za Private Mtoto asisimamishwe au Kufukuzwa.
Ada ya Private huwa inatumikaje?
Ujenzi wa miundombinu inategemea Ada hizi kuanza madarasa hadi ofisi.
Chakula cha wanafunzi kinategemea ada hizi.
Mishahara ya waalimu wanalipwa na ada hizi.
Stationary zinategemea ada hizi
Mishahara ya walinzi,wapishi wanalipwa na ada hizi.
Mafuta ya magari yanatokana na ada hizi
Wasipolipa maji wanakatiwa maji
Umeme nao ukiisha wanakatiwa papo hapo
Kila kitu kwenye Shule za Private hakiendi bila michango ya wazazi.
Kauli hii haijengi Bali inabomoa Shule hizi za private, ninavyowajua watanzania toka kauli hii ilivyotoka watasua sua sana kulipa kwa kuwa wanajua hawatasumbuliwa.
Tumefanikiwa kuleta mgogoro kwenye Shule zetu za Serikali kwa kutoa nyaraka ambazo hazieleweki. Wazazi kwenye Shule za serikali wanasua sua haswa kuchangia vyakula vya watoto wao na majukumu mengine ambayo yameainishwa na waraka wa Elimu.
Kwetu kumetushinda tumehamia kwa wenzetu, huku Private wazazi wakisikiliza kauli hii mambo yanaenda kukwama asubuhi kabisa. Mzazi mpaka anaamua kumpeleka Mwanafunzi wake Private alishajipima akaona anamudu na akasaini mkataba.
Hii ni biashara sio Huduma ya Bure, Ni sawa na mtu aje apande Bombadia zetu akuambie nitalipa siku nikipata. Je zitajiendeshaje? Ni mtanzania gani anaweza kufanya hivyo na akasamehewa?
Tunaingilia sana Sector binafsi badala ya Serikali kufanya hivyo iboreshe mazingira ya utoaji huduma zake ili wananchi Wengi wasaidike serikalini kuliko huko private.
Shule za Serikali zina changamoto kibao kwa sasa kama vile....
Uhaba wa vyumba vya madarasa mwaka huu.
Wanafunzi hawajaripoti huko mtwara na Lindi.
Kuna watu wanasomea chini ya mikorosho na wengine kukalia mawe hakuwahi kwenda kushughulika nao.
Kuna uhaba mkubwa wa matundu ya vyoo kwa shule zetu pamoja na uhaba wa watumishi wengine hakuwahi kwenda kushughulika nao.
Matatizo ni mengi sana Serikalini uchakavu wa Miundombinu, hawajawahi kuahngaika navyo.
Shule kuwa na uhaba wa waalimu nk... Haya yote Waitara kayaacha kaenda kutengeneza tatizo mahali ambapo wala kulikuwa hakuna tatizo. Ya serikali yamemshinda kakimbilia Private.
Siwatetei ila naomba kwa mbali jinsi wazazi watakavyotumia kauli hiyo vibaya, naona mishara ya waalimu ikisusua sua, naona wakifunga shule zao na kuua Ajira za maelfu ya watanzania.
Sijui pale International school of Tanzania nao Tamko hili linawahusu kuwa walipe siku wakipata. Pale Feza mfano wazazi walishakaa wakaamua wakasainiana wewe unatokea ulikotokea utafikiri vikao vya hawa wazazi ukikaa unakuja na kauli yako binafsi....
Tumeacha mambo ya msingi tukarukia mambo marahisi sana kama ilivyo kawaida yetu.
Kama tunaona Wazazi wanateseka tuondoe Kodi kabisa kwenye hizi shule Binafsi ili walipe Ada kidogo basi iwe ni sehemu ya Huduma Serikali inatoa.

Mwandishi: Ole Mushi.
0712702602
 
Kama vile serikali ilivyomkatalia manji Yanga kwa kudai anziishe Timu yake basi nayo serikali isiingilie shule binafsi ikitaka ijenge zake ambazo inaruhusu wazazi kuchekewesha ada!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom