Waitara: Serikali mnatoa kibali mahusiano ya jinsia moja?

Waitara: Serikali mnatoa kibali mahusiano ya jinsia moja?

Atukuzwaye

Senior Member
Joined
Oct 5, 2026
Posts
188
Reaction score
245
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii jinsia wanawake na Makundi Maalumu Maryprisca Mahundi amesema Serikali haitoi uhalali wa uvunjifu wa maadili kwa wananchi wake.

Mahundi amesema hayo Bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Tarime Vijijini Mwita Waitara aliyetaka kujua uhalali wa shughuli za watu wanaojijusisha na mahusiano ya jinsia moja jambo ambalo linaharibu maadili ya Mtanzania. Aidha Mahundi amewataka wazazi na walezi kushirikiana na Serikali katika kulinda maadili ya Mtanzania kwa kuzingatia mila na desturi.

Hayo yamejiri leo November 2, Bungeni jijini Dodoma katika mkutano wa tano kikao cha tano bunge la 13 linaloendelea Bungeni jijini Dodoma.

Soma pia: Mbunge Kampala: Dar ni Kiwanda kikubwa sana cha kuzalisha Mashoga, nini kauli ya Serikali?

 
Back
Top Bottom