Naibu Waziri Mavunde alazwa hospitalini Morogoro, anasumbuliwa na homa kali


Dar es Salaam, Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu, Anthony Mavunde amelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro akisumbuliwa na homa kali.

Akizungumza na MCL Digital, Mavunde amesema alipelekwa hospitalini hapo usiku wa kuamkia leo Jumapili Machi 18, 2018 baada ya kujisikia vibaya.

“Nililetwa hapa usiku na kwa sasa naendelea kupatiwa matibabu,” amesema Mavunde.

Chanzo: Mwananchi
CORONA
 
Back
Top Bottom