TANZIA Gregory Teu aliyewahi kuwa Naibu Waziri wa Fedha, Viwanda, Naibu Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali na Mbunge wa Mpwapwa, afariki dunia

Ngariba1

JF-Expert Member
Jan 12, 2017
1,702
3,454
Aliyewahi kuwa Mbunge wa Mpwapwa 2010- 2015 , Naibu waziri wa fedha, Naibu waziri wa viwanda, Naibu Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali katika serikali ya awamu ya nne na mwenyekiti wa bodi ya KADCO Mh. Gregory Teu afariki Dunia leo hii.


Teu.jpg

Taarifa zaidi:
Mpwapwa. Mbunge wa zamani wa Mpwapwa mkoani Dodoma nchini Tanzania, Gregory Teu amefariki dunia usiku wa kuamkia leo baada ya kujisikia vibaya akiwa kikaoni.

Akizungumza leo Jumatatu Januari 25 2020, Msemaji ukoo wa Teu Stanley Mbijili amesema Teu alikuwa kwenye kikao cha bodi ya Kampuni ya Maendeleo ya Kiwanja cha Ndege cha Kilimanjaro (KADCO) ambacho yeye ni mwenyekiti wake.

Mbijili amesema marehemu alifariki saa 9.00 alfajiri usiku wa kuamkia leo wakati akiendelea na matibabu katika hospitali ambayo bado haijafahamika.

“Tunajua kuwa marehemu alienda Arusha kwenye kikao cha Bodi kwa sababu yeye alikuwa ni Mwenyekiti wa bodi hiyo ila hatujajua alikufa katika hospitali gani,”amesema.

Amesema utaratibu wa kusafirisha mwili wake utafanyika Januari 27 (kesho kutwa ) kutoka Arusha kwenda Wilayani Mpwapwa na kwamba mazishi yatafanyika Jumatano (Januari 28) katika makuburi yaliopo katika viwanja vya Kanisa la Watakatifu Wote Vighawe.

Amesema kuwa Teu alikuwa akisumbuliwa na shinikizo la damu na sukari mara kwa mara.

Teu aliwahi kuwa Mbunge wa jimbo la Mpwapwa (CCM) kati ya mwaka 2010 hadi 2015 na kuteuliwa na Rais Jakaya Kikwete kuwa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango na baadaye Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara.

Pia Teu aliwahi kuwa Naibu Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kabla ya kuchaguliwa kuwa mbunge wa Mpwapwa katika uchaguzi mkuu mwaka 2010.

Aliteuliwa kuwa mwenyekiti wa bodi hiyo Oktoba 17 mwaka 2017 baada ya Rais John Magufuli kutengua uteuzi wa aliyekuwa mwenyekiti wa bodi hiyo, Balozi Hassan Kibelloh.

Chanzo: Gazeti Mwananchi
 
Huyu aliwahi kuwa mbunge wa mpwapwa kweli?
Mzee G, Lubeleje ambae alikuwa mbunge wa Mpwapwa kwa miaka yote Hadi mwaka 2020,alipo katwa CCM,alikuwa mbunge wa Jimbo gani?
hapoo, na mimi nikadhani anamzungumzia mh Lubeleje!.
 
Huyu aliwahi kuwa mbunge wa mpwapwa kweli?
Mzee G, Lubeleje ambae alikuwa mbunge wa Mpwapwa kwa miaka yote Hadi mwaka 2020,alipo katwa CCM,alikuwa mbunge wa Jimbo gani?
2010 -15 alimwangusha Lubeleje! GML akaja akarudi tena 2015-2020
 
Back
Top Bottom