Naibu Waziri aikalia kooni TANESCO | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naibu Waziri aikalia kooni TANESCO

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by PROFESA KYANDO, Aug 31, 2012.

 1. PROFESA KYANDO

  PROFESA KYANDO Member

  #1
  Aug 31, 2012
  Joined: Jul 24, 2012
  Messages: 81
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [​IMG][h=2][/h] Ijumaa, Agosti 31, 2012 06:30 Na Benjamin Masese

  *Aiagiza isikate umeme ovyo * RC Simbakalia amwaga ‘kilio’
  SERIKALI imeliagiza Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), kuacha mara moja kukata umeme katika taasisi zote ambazo zinatoa huduma muhimu kwa jamii.

  Kauli ya Serikali imetolewa jana na Naibu Waziri wa wizara hiyo, George Simbachawene wakati alipomtembelea Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Joseph Simbakalia, ili kupata taarifa ya maendeleo sekta ya nishati mkoani humo.

  “Kuanzia sasa, naiagiza TANESCO kuacha mara moja tabia ya kukata umeme katika taasisi ambazo zinatoa huduma nyeti kwa taifa… hii ni kutokana na ukweli kwamba, mambo muhimu hurudi nyuma,” alisema Waziri Simbachawene.

  Waziri Simbachawene yupo mkoani Mtwara, kwa ajili ya kukagua maendeleo ya miradi ya nishati, ikiwa ni pamoja na maandalizi ya ziara ambayo inatarajiwa kufanywa na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo.

  Akitoa taarifa ya upatikanaji wa nishati, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Joseph Simbakalia, alisema anasikitishwa mno na tabia ya shirika hili kukata umeme mara kwa mara.

  “Tunasikitishwa mno na tabia ya TANESCO kukata umeme mara kwa mara, jambo hili linarudisha nyuma maendeleo ya mkoa na taifa…tunaomba suala hili mliangalie sana,” alisema Simbakalia.

  Alisema shirika hilo, limekuwa likikata umeme katika maeneo nyeti kama vile idara ya elimu, maji na afya, jambo ambalo limekuwa likirudisha nyuma shughuli za maendeleo.

  Alisema anasikitishwa na ucheleweshaji mkubwa unaofanywa na TANESCO mkoani humo, kurudisha umeme pindi unapokatika.

  Kutokana na maelezo hayo, Waziri Simbachawene alitoa agizo kwa shirika hilo, kusitisha oparesheni hiyo nchi nzima.

  Kuhusu madeni ambayo shirika hilo, linawadai wateja wake, Waziri Simbachawene alisema, ni lazima walipe madeni yao kwa wakati ili shirika liweze kujiendesha.

  “Wateja wa TANESCO, lazima walipe madeni…mpango wa kudai madeni kwa wateja ni muhimu, siuzuii hata kidogo, nawashauri kabla ya kuchukua uwamuzi wa kukata umeme, wawasiliane na ofisi za wakuu wa mikoa, ili kujua kama taasisi hizi zinaweza kulipa.

  Akitoa ufafanuzi kuhusu kilio cha wananchi wa Mtwara, kuhusu kutosomewa mapato na matumizi na mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Mtwara, Waziri Simbachawene alisema, kosa hilo ni kubwa.

  “Nimepokea malalamiko ya wananchi kutosomewa mapato na matumizi, namuagiza mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Mtwara, kuweka wazi mapato yoye yanayotokana na gesi na kuhakikisha vijiji vilivyo karibu na miradi ya uzalishaji, vinapewa kipaumbele katika gawio la mapato, ili kuondokana na migogoro ya mara kwa mara,” alisema.

  Kabla ya kutembelea ofisi ya mkuu wa mkoa, Waziri Simbachawene alikutana na wananchi wa Kijiji cha Msimbati kilichopo Wilaya Mtwara na kusikiliza kero zao.

  [h=4]Toa Maoni yako kwa habari hii[/h]
   
 2. G

  Gwakisa Mwandule JF-Expert Member

  #2
  Aug 31, 2012
  Joined: Jun 20, 2012
  Messages: 520
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Huyu ni mbunge wa Kibakwe jimbo hilo lipo mkoani Dodoma wilaya ya mpwapwa kama sikosei inasemekana wananchi wa huko hawamkubali hata kidogo maana alishawahi kuwaambia haoini sababu ya kuwapa maendeleo wahamiaji ambao ni wahehe japo na yeye ni muhehe,Hafahamiki sana kwenye siasa za makundi lakini jamaa ni bomu hana lolote kielimu maana ana FTC then anawadanganya watu eti ana degree ya sheria.Bensoni kigaila ambaye ni mkurugenzi wa M4C ndiye alipaswa kuwa mbunge wa pale wakachakachua ndo gamba chawene akawa mbunge!Kwa huyu tusitegemee lolote la maana kutokana na jamaa kuwaza mademu muda woooote wa maisha yake!Gamba,dhaifu,liwalo na liwe CCM wanatokota
   
Loading...