PreGE2025 Naibu spika: Tume ya sasa ni bora kuliko iliyowapa upinzani ushindi 2015

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Just Pray

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,142
Reaction score
4,779
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mussa Azzan Zungu, ameviita vyama vya upinzani nchini Tanzania kushiriki katika Uchaguzi Mkuu wa baadaye mwaka huu, akieleza kuwa hata mabadiliko wanayoyataka na kuyahimiza ya kisheria na kimfumo yatapatikana ndani ya bunge hilo na siyo barabarani.

Naibu Spika amebainisha hayo jioni ya Aprili 30, 2025 wakati akiishukuru Wizara ya Katiba na Sheria kwa hotuba ya Bajeti waliyoiwasilisha mapema asubuhi pamoja na hitimisho la mjadala wa hotuba hiyo walioufanya, akieleza kuwa kwasasa Tume ya Uchaguzi ni bora zaidi kuliko ile ambayo ilifanikisha Bunge kuwa na wabunge wa Vyama pinzani takribani 112 kutoka vyama mbalimbali.

Akimpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kujivua madaraka aliyokuwa nayo awali kwenye uteuzi wa viongozi mbalimbali wanaosimamia uchaguzi Mkuu, Naibu Spika amesisitiza kwa wizara pia umuhimu wa kwenda kuwaeleza wananchi mabadiliko mbalimbali ya sheria za uchaguzi yaliyofanyika sambamba na ushiriki wa vyama vya upinzani ulivyokuwa wakati wa mchakato wa mabadiliko hayo yaliyofanywa na Bunge na mamlaka nyingine mbalimbali.

Tatizo kisukari cha akili.
Mm nikienda Oman kesho naweza kuchaguliwa kuwa naibu speaker???
 
View attachment 3321782
Uchaguzi wa Nov 2024 ulikuwa chini ya tume ipi?

#NoReformsNoElection
 
Mwizi mwingine wa kura huyooooo!!
 
Back
Top Bottom