Kumekuwa na maswali mengi tangu uteuzi wako kuwa naibu mwanasheria mkuu, siku chache baadaye ukachukua fomu ya kugombea uspika. Mara ukatangaza kujitoa kwenye kinyang'anyiro cha uspika na siku chache baadaye ukateuliwa kuwa mbunge kisha ukachukua fomu ya kugombea unaibu spika.
Kisha tukaanza kushuhudia wengi wa wagombea wakijitoa na akina mhe. Zungu waliokuwa wamejipa matumaini ya kupata nafasi hiyo kabla yako wakazungushwa na kuambulia patupu. Wengi tulijipa majibu kwa maswali mengi tuliojiuliza juu ya ulazima wa wewe kuwa spika ama naibu spika.
Kwamba yawezekana una weledi mkubwa juu ya masuala ya kibunge ama una uadilifu usiotiliwa shaka.
Sasa kinachoendelea bungeni kinatoa taswira tofauti. Kwamba ama uliwekwa kimkakati kulinda maslahi fulani kwa kubinya uhuru wa sauti zisizotakiwa kusikika na wakubwa.
Ulianza na swala la bunge kutokuwa live. Kuna uzi humu umeandika kuwa swala hili umelitekeleza wewe kwa maelekezo ya wakubwa huku bosi wako (spika) akiwa haliafiki. Na hata katika vikao vya chama (ccm) wabunge wengi hawakuliafiki kabisa. Lkn mwishowe ni naibu spika na waziri Nape ndiyo mliosimama mkatoa msimamo kuwa itakuwa hivyo.
Tulimsikia pia mhe Godbless Lema akikutuhumu kutokumshirikisha boss wako (spika) ktk maamuzi ya kupeleka fedha kwa rais zilizotokana na kubana matumizi ya bunge.
Na sasa hili linaloendelea sasa la kutokuwapa nafasi wabunge wanawake kama wewe pale wanapoomba nafasi ya kukemea udhalilishaji wanaofanyiwa bungeni. Japo wanatoka vyama pinzani lkn suala la mwanamke kudhalilishwa halikupaswa kuwa na itikadi.
Nikuombe mhe. naibu spika tudhihirishie kuwa ulitafutiwa nafasi hiyo kwa udi na uvumba kwasabb ya weledi wako na si vinginevyo. Simama ktk mstari wa haki.