mcfm40
JF-Expert Member
- Nov 2, 2010
- 4,452
- 3,151
Tangu wabunge wa upinzani waanze kumsusia vikao anavyoviongoza, naye amelazimika kuongoza vikao vingi vya bunge ili kuwakomoa upinzani. Je wanamshauri kufanya hivi hawaoni wanafamfanya naye awe kama yupo kwenye adhabu?
Bunge lina wenyeviti watatu lakini tangu wabunge wa upinzani wasuse imebidi wakae pembeni na kumwachia naibu spika peke yake aongeze vikao peke yake bila kupumzika kama ilivyokuwa kawaida.
Kipindi hiki ambapo spika hayupo naibu spika ndiye anakuwa na majukumu ya kufanya mambo mengi ndani na nje ya bunge. Lakini sasa imembidi naibu spika kukaa bungeni muda wote ili kuwakomoa UKAWA huku shughuli nyingine za kiofisi zikidorora!
Hivyo namwona NS naye kama yupo kwenye adhabu ambapo anashindwa kufanya shughuli zake katika mtiririko wa kawaida wa siku zote!
UKAWA endeleeni kukaza mpaka aombe poo!