Naibu Spika aagiza wabunge watakaokuwa wanasusia Bunge kutolipwa posho

Michael Amon

JF-Expert Member
Dec 22, 2008
8,768
3,621
Kutokana na wabunge wengi waCCM kulalamika na kuomba mwongozo wa spika juu ya wabunge wanaotoka nje baaada ya kujisajili, naibu spika amelipitia suala hilo na hatimaye kuja na hitimisho kuwa wabunge hao hawatapokea posho zao kwa kipindi chote ambacho hawakuhudhuria vikao.

Amesema uamuzi huu ameufikia baada ya kupitia maamuzi mbalimbali yaliyotolewa na bunge juu ya wabunge ambao walikuwa wanaondoka bila kuchangia mjadala ambapo tarehe 08/04/2008 wabunge wa chama cha CUF walitoka bungeni na kususia shughuli zilizokuwa zimepangwa na kiti kilitoa uamuzi wa kutowalipa posho kwa siku zote watakazokuwa nje


 
upload_2016-6-8_18-35-36.jpeg


Wakati naibu spika wa jamhuri ya muungano wa tanzania akihairisha bunge jioni ya leo,amefuta rasmi posho zote za wabunge wa ukawa ambao wa mekuwa wakisusia bunge,baada ya dua ya asubuhi.

Naibu spika ametoa maamuzi kwamba AMEFUTA RASMI POSHO ZOTE ZA WABUNGE WAMBAO WANTOKA BUNGENI BILA RUHUHA.

na amesisitiza kwamba kutoka nje hakuvumiliki.
 
na sheria za kudumu za bunge amezikiuka kwa kuwa na hamasa za miongozo je hili tamko limefuata sheria ipi ya kudumu ya bunge ama kikao kani kilikaaa kutengua kanuni za bunge.yasije yakawa ya sukari
 
Kauli yake Naibu Spika:
Naagiza kwamba wabunge wote watakaokuwa wanasaini kisha kutoka nje ya Ukumbi hawatalipwa posho kwa siku zote walizotoka.
Hana uwezo huo kwani kulipwa kwa mbunge siyo lazima awe ndani ya jengo,ili mradi yupo kwenye majukumu ya kibunge kulipwa ni lazima labda atunge katiba yake
 
Awamu hii hakuna kususa,ukisusa hawakubembelezi .

JK alikuwa anawabembeleza upinzani wakamuita dhaifu, Upinzani watamkumbuka sana JK . Itabidi wabunge wa UKAWA waondoke Dodoma maana watakufa njaa.
Wabunge wetu siye CCM tunawapenda kwa kutetea posho zao
 
hii ndio njia pekee ya kumsaidia maskini anayelipa kodi na kuliwa na watu wakiwa hotelni.
sasa kama kuna watu yanatoka kwa pressure za vyama vyao hasa uanachama wake ndo wachague kimoja.....wake kwenye mikopo yenye riba.respect Dr.TULIA
 
Hana uwezo huo kwani kulipwa kwa mbunge siyo lazima awe ndani ya jengo,ili mradi yupo kwenye majukumu ya kibunge kulipwa ni lazima labda atunge katiba yake
Eti kwa mujibu wake, hao wabunge wakitoka hawaendi kwenye majukumu ya kibunge. Yaani (wengine wanaenda kunywa kahawa na wengine wanaenda kuchapa usingizi)
 
Back
Top Bottom