Kauli ya Tundu Lissu juu wabunge 19 waliofukuzwa

BAVICHA Taifa

Senior Member
Jul 25, 2013
117
661
Mbunge anapopoteza sifa ya kuwa mbunge, whether kwa kufukuzwa uanachama au kwa sababu nyingine yoyote, hastahili kuendelea kuwa mbunge kwa siku moja zaidi.

Na hali hiyo inaendelea hadi hapo Mahakama Kuu, au Mahakama ya Rufaa ya Tanzania, itakapoamua vinginevyo.

Mimi nilivuliwa ubunge na Spika Ndugai. Nilikwenda Mahakama Kuu kuomba ruhusa ya kupinga uamuzi wa Spika mahakamani.

Niliponyimwa ruhusa hiyo nilikata rufaa katika Mahakama ya Rufaa. Rufaa hiyo haikusikilizwa hadi Bunge la 11 linakwisha muda wake.

The fact kwamba nilikuwa na rufaa mahakamani haikubadilisha status yangu ya kutokuwa na sifa ya kuendelea kuwa mbunge.

Mheshimiwa Lema alivuliwa ubunge na Mahakama Kuu. Alitolewa nje ya Bunge kwa kukosa sifa kutokana na kuvuliwa ubunge. Alikata rufaa Mahakama ya Rufaa, lakini aliendelea kuwa nje ya Bunge hadi Mahakama ya Rufaa ilioamua kwamba alikuwa mbunge halali.

Wabunge tisa wa chama cha CUF walifukuzwa uanachama wa kilichokuwa chama chao. Walitolewa Bungeni kwa kukosa sifa ya kuendelea kuwa wabunge.

Wabunge hao walifungua kesi Mahakama Kuu kupinga uamuzi wa kuwafukuza uanachama. Kufungua kesi peke yake hakukuwarudisha Bungeni.

Mifano ya aina hii ni mingi sana katika historia yetu ya kisiasa na kibunge.

Spika Tulia Ackson anasemekana kuwa na PhD ya sheria. Alikuwa mwalimu wa sheria Chuo Kikuu na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Anajua sheria za nchi yetu na misingi yake. Uamuzi wake ni wa kisiasa; kwa sababu za kisiasa.

Ni wazi kwamba suala la COVID-19 ni suala la mfumo mzima wa utawala. Ikulu ya Magufuli ilihusika katika kuwaingiza Bungeni, na sasa Ikulu ya Samia inahusika na kuendelea kwao kuwa Bungeni.

Kwa Katiba na sheria zetu kama zilivyo sasa, Rais ndiye anayeamua malipo ya mishahara na posho za wabunge. COVID-19 wako Bungeni na wataendelea kuwa Bungeni sio kwa sababu wana kesi mahakamani, bali kwa sababu Samia anawalipa posho na mishahara yao.

Tuelekeze nguvu na mashambulizi yetu kunakostahili: kwa Rais Samia Suluh Hassan.

images%20(1).jpg
 
Tulia anasema kuanzia leo anafunga mjadala kuhusu hao wanawake 19, na kama yupo yeyote anayetaka maelezo yao amuone yeye Spika, sijui kwanini anawafunga watu midomo.

Hapa ni wazi kuna mchezo unachezwa, na inawezekana kabisa Samia akawa miongoni mwa wachezaji hao.

Ikumbukwe Samia alikuwa msaidizi wa Magufuli, inawezekana nae aliubariki huu mpango wa hawa wanawake 19 kwa manufaa ya CCM ndio maana bado anawalinda.

Nawashauri Chadema na Mbowe huu ni wakati wenu kususia vile vikao vya "maridhiano" na Samia kule ikulu, hawa watu wanaonesha wazi tena kwa vitendo hawana nia ya kutibu majeraha, wanawadharau.
 
Hapa ni wazi kuna mchezo unachezwa, na inawezekana Samia akawa miongoni mwa wachezaji hao.

Chadema na Mbowe huu ni wakati wenu kususia vile vikao vya maridhiano na Samia kule ikulu, hawa watu wanaonesha wazi tena kwa vitendo hawana nia ya kutibu majeraha, wanawadharau.
Ndo uelewe hangaya haaminiki kwenye jambo lolote- ulaghai mwingi, kumwelewa inahitaji akili kidogo tu, inshort ni kwamba hayuko real kwenye jambo lolote linalohusisha nia njema.
 
Back
Top Bottom