Naibu Meya (CHADEMA) matatani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naibu Meya (CHADEMA) matatani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, May 12, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  May 12, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  * Tatizo ni kuwa chama tawala bado kina Mamlaka kwenye Vyombo Vya Usalama; Bado Ofisa Mwandamizi wa Polisi anachaguliwa na Rais; This must stop to have a fair and balance rule.  Thursday, 12 May 2011 19:08


  NA PETER KATULANDA, MWANZA

  NAIBU Meya wa Jiji la Mwanza, Charles Chinchibela (CHADEMA), ameingia matatani baada ya kudaiwa kumtishia maisha mwananchi wake. Chinchibela, ambaye ni Diwani wa Kata ya Mahina, amefunguliwa jalada la uchunguzi Polisi lenye namba MW/RB/3782/2011 na IR/2743/2011. Habari kutoka ndani ya Jeshi la Polisi mkoani hapa, zimesema Chinchibela atafikishwa mahakamani wakati wowote baada ya uchunguzi kukamilika. Ilidaiwa kuwa Naibu Meya alimtishia maisha Felician Burakali, mkazi wa Bugarika katika Kata ya Mahina,
  ambako anaoingoza Aprili 12, mwaka huu, akiwa eneo la Mahakama ya Wilaya ya Mwanza. Habari zimedai kuwa chanzo cha Burakali kutishiwa maisha na Meya huyo ni uamuzi wake kwa kumfikisha mahakamani mkazi mwenzake aitwaye Kahawa, ambaye awali alimtishia kumuua kwa kumkata panga mbele ya Ofisa Mtendaji wa Mtaa wa Mahina. “Kahawa alikamatwa na kufikishwa katika Mahakama ya Mwanzo Mwanza na kudhaminiwa na Chinchibela, ambaye kwa mujibu wa mlalamikaji, baada ya dhamana alimtishia atamfuatilia hadi mwisho wa maisha yake,” kilisema chanzo chetu.
  Kamanda wa Polisi mkoani hapa Simon Sirro, alisema jana tuhuma hizo bado zinaendelea kuchunguzwa kabla ya mtuhumiwa kufikishwa mahakamani.
  Pia, alisema kuwa walimkamata na kumhoji Chinchibela juu ya tuhuma hizo za kumtishia mtu maisha
   
 2. z

  zamlock JF-Expert Member

  #2
  May 12, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 3,849
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  ccm na mfumo dume
   
 3. M

  MPG JF-Expert Member

  #3
  May 12, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 483
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hawo ni wakoloni weusi CCM
   
 4. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #4
  May 13, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Chadema ni chama cha shari always. Action speak louder than words. Thanks Lod for showing us. Now the truth will set us free.
   
Loading...