Naibu Katibu wa Bunge:Hakuna kanuni za Bunge zinazozuia mtu kuingia Bungeni akiwa amelewa

Salary Slip

Platinum Member
Apr 3, 2012
49,321
152,121
Akiingoe na gazeti la Nipashe,Naibu Katibu wa Bunge,John Joel amesema hakuna kifungu chochote cha kanuni za Bunge zinazomzuia mtu kuingia Bungeni akiwa amelewa.

"Kanuni zinahusiana na uendesha wa shughuli za Bunge,hizi za Maadili ni kanuni za Maadili ambazo zinatakiwa kutungwa ili kudhibiti hali hiyo ",alisema Joel.

Chanzo:Nipashe online

Kwa mujibu wa habari hii,mbunge wa Sumve, Richard Ndasa alimsihi mara tatu Kitwanga asiingie Bungeni kwasababu alikuwa na kila dalidali za kulewa lakini Kitwanga alikataa na hata baada ya kikao cha Bunge kwisha, Ndasa alijaribu kumshika mkono Kitwanga ili amuondoe katika viwanja ya Bunge lakini Kitwanga alimkimbia.

Kwa mijibu wa maelezo ya Ndassa katika habari hii,baada ya Kitwanga kumkimbia,Ndasa alimfuata dereva wa Kitwanga na kumwambia amuondoe Kitwanga katika viwanja vya Bunge ila Kitwanga alikataa kuingia ndani ya gari.Ndasa ni mwenyekiti wa wabunge wa mkoa wa Mwanza.

Baada ya kusoma haya maelezo ya Ndasa naanza kujiuliza hivi Kitwanga ni nini kilimsibu mpaka kufanya haya yote au alifanya tu makusudi ili haya yatokee?Mbona hii kitu haingii akilini?
 
Siku za yeye kuwa waziri zilikuwa zimekwisha, amshukuru Mungu kumuachia uhai wake
 
Upumbavu huu na katibu wa bunge ni kilaza..Kwani bunge si mahala pa kazi??pumbavuuu ni Ray"Maji" s voice.
Acha kumtukana bora yeye kawa muwazi kuwa Bunge halina kanuni inayozuia ulevi kwani angeweza kukaa kimya tu kama jinsi viongozi wengine wa Bunge walivyoamua kukaa kimya juu ya swala hilo mpaka sasa.
 
Basi hapo hakuna tatizo nimbunge kama kawaida
Ila uwaziri ndio imekula kwake
 
Akiingoe na gazeti la Nipashe,Naibu Katibu wa Bunge,John Joel amesema hakuna kifungu chochote cha kanuni za Bunge zinazomzuia mtu kuingia Bungeni akiwa amelewa.

"Kanuni zinahusiana na uendesha wa shughuli za Bunge,hizi za Maadili ni kanuni za Maadili ambazo zinatakiwa kutungwa ili kudhibiti hali hiyo ",alisema Joel.

Chanzo:Nipashe online

Kwa mujibu wa habari hii,mbunge wa Sumve, Richard Ndasa alimsihi mara tatu Kitwanga asiingie Bungeni kwasababu alikuwa na kila dalidali za kulewa lakini Kitwanga alikataa na hata baada ya kikao cha Bunge kwisha, Ndasa alijaribu kumshika mkono Kitwanga ili amuondoe katika viwanja ya Bunge lakini Kitwanga alimkimbia.

Kwa mijibu wa maelezo ya Ndassa katika habari hii,baada ya Kitwanga kumkimbia,Ndasa alimfuata dereva wa Kitwanga na kumwambia amuondoe Kitwanga katika viwanja vya Bunge ila Kitwanga akikataa kuingia ndani ya gari.Ndasa ni mwenyekiti wa wabunge wa mkoa wa Mwanza.

Baada ya kusoma haya maelezo ya Ndasa naanza kujiuliza hivi Kitwanga ni nini kilimsibu mpaka kufanya haya yote au alifanya tu makusudi ili haya yatokee?Mbona hii kitu haingii akilini?
Pengine ni stress.
 
Sheria za bunge au kanun zinaweza kuwa sahih hivyo ila yeye amefukuzwa kwa nafasi au kwa kutumia sheria za mtumish wa umma
Well said. Pale alitumwa na serikali kikazi si bunge. Mihimili miwili tofauti yenye sheria, taratibu na kanuni tofauti.
 
Upumbavu huu na katibu wa bunge ni kilaza..Kwani bunge si mahala pa kazi??pumbavuuu ni Ray"Maji" s voice.
Acha kumtukana bora yeye kawa muwazi kuwa Bunge halina kanuni inayozuia ulevi kwani angeweza kukaa kimya tu kama jinsi viongozi wengine wa Bunge walivyoamua kukaa kimya juu ya swala hilo mpaka sasa.
Kama hata bunge lina ubora duni kiasi hiki basi kuna kazi ngumu ya kuiendeleza TZ. Serikalini Magufuli anatumbua watu kama huyu Naibu katibu wa Bunge, Huko Bungeni nani anawatumbua?

Huwezi kutunga kanuni ya Ulevi, Kanuni ya kufunga zip ya suruali, Kanuni ya kubrashi viatu, kanuni ya ... kuna mambo hayaruhusiwi kwa nature ya kazi, finito! TZ hakuna kazi inayofanywa na mtu aliyelewa sasa yeye anataka bungeni mpaka iwe ktk kanuni! Shiiit!

Kama watatunga kanuni halafu jamaa akaja na chupa ya konyagi bungeni, bila hata kuinywa itaruhusiwa? au kwa upuuzi kabisa, badala ya leso akaja na chupi ya mkewe, nayo atasubiri watunge kanuni? Bunge hoi kabisa!!! NIMECHUKIA UWEZO MDOGO WA MAAFISA WA BUNGE.
 
Hii issue mimi nina mashaka nayo sana maana ni kama movie tu tena movie ya vichekesho.
Kuna wanaodai kwamba kitwanga hakunywa chochote zaidi ya chai ya rangi , ila alijifanya kalewa ili dili litimie ! ( tuichukulie kama tetesi kwanza ) , nina nzi wawili , mmoja bungeni mwingine home affairs .
 
Back
Top Bottom