Nahofia Mabadiliko! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nahofia Mabadiliko!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kijakazi, Sep 22, 2012.

 1. Kijakazi

  Kijakazi JF-Expert Member

  #1
  Sep 22, 2012
  Joined: Jun 26, 2007
  Messages: 3,546
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 135
  Nawapenda CHADEMA, napenda kuwasikiliza, saa nyingine nahudhuria Mihadhara yao, lakini mimi binafsi nina tatizo moja, nahofia mabadiliko, nahofia nini kitakuja baada ya CCM kuondoka, pamoja na ukweli kwamba nimechoshwa na maovu ya CCM (viongozi) lakini angalau nawajua CCM na najua wana mipaka ya maovu yao, kuna baadhi ya vitu hawawezi kufanya, lakini Chama kipya kabisa nahofu sana kwa maana najua wataleta mabadiliko lakini sijui ni mabadiliko gani hayo, inawezekana Mungu saidia yakawa mazuri au pia inawezekana Mungu pisha mbali yakawa mabaya sana na tukashindwa kurudi tulipokuwa mwanzo kabla ya wapinzani kuingia, hiyo ndio Hofu yangu ingawaje napenda Maisha yetu yabadilike lakini pia nina kahofu kaliko jificha!
   
 2. B

  Bubona JF-Expert Member

  #2
  Sep 22, 2012
  Joined: Aug 31, 2011
  Messages: 449
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Hofu itaendelea kukutawala mpaka utakapoamua kuishinda; vinginevyo utaendelea kuwa Kijakazi!!
   
 3. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #3
  Sep 22, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,629
  Likes Received: 9,847
  Trophy Points: 280
  the greatest fear in this world is fear itself.....
   
 4. PRINTABLUE

  PRINTABLUE Member

  #4
  Sep 22, 2012
  Joined: Jul 15, 2012
  Messages: 79
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hofu na mashaka ni mizizi ya dhambi. Ishinde dhambi hiyo kwa kukubali mabadiliko.
   
 5. Kijakazi

  Kijakazi JF-Expert Member

  #5
  Sep 22, 2012
  Joined: Jun 26, 2007
  Messages: 3,546
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 135
  Kwa hiyo wewe hauna hofu hata kidogo kwa usichokijua?
   
 6. Thanda

  Thanda JF-Expert Member

  #6
  Sep 22, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 1,915
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  The Great fear (la Grande Peur) to fear is fear itself - Franklin D. Roosevelt, the Americans president in 1933, during the Great Depression. Hivyo basi ni vizuri kuihofu hiyo hofu uliyo nayo na kuishinda, kuliko hofu ya kutawaliwa na Chama kipya. Na wala si kipya, sema chama kigeni katika nyanja za kiutawala...Ila tafakari sana na tena kwa umakini-Kama chama kikonwe kimeshindwa kuidhibiti hali na "chama kigeni" kimeonesha uwezo mkubwa na tena unaokubalika ndani na nje, kwanini uwe na hofu. Ihofie hiyo hofu uliyo nayo na wala si chama kwani chama si mtu mmoja anayeweza kuwa na maamuzi ya kidikteta.
   
 7. Autorun

  Autorun JF-Expert Member

  #7
  Sep 22, 2012
  Joined: Mar 21, 2008
  Messages: 556
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  usiwe na hofu na mabadiliko mabadiliko sahihi na yenye nguvu yana anza na wewe mwenyewe kua tayari kuyakubali mabadiliko............ AMNI MABADILIKO YAKWELI YA TANZANIA YENYE NEEMA KWENDA TANZANIA ILIYO NEEMEKA HAYATALETWA NA CHADEMA, CCM, ADC, CUF etc BALI WATANZANIA WALIO TAYARI KUBALI MABADILIKO NA WATHUBUTU.......... CHADEMA ni upepo tu kuelekea mabadiliko wape nafasi
   
 8. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #8
  Sep 22, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Hama NCHI rudi baada ya MABADILIKO...
   
 9. Kijakazi

  Kijakazi JF-Expert Member

  #9
  Sep 22, 2012
  Joined: Jun 26, 2007
  Messages: 3,546
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 135
  Kwa nini kuhofia kitu usichokijua iwe Dhambi? sijasema kwamba sikubali mabadiliko ila nimesema tu kwamba kuna kahofu kalikojificha ndani yangu ya kitu nisichokijua, hata Yesu alipokuja na akawa anatagaza neno la Mungu kuna watu wengi tu walimhofia sio kwa sababu alikuwa anahubiri upuuzi bali ni kwa sababu alikuwa anahusbiri vitu vipya na watu wengi walikuwa wanahofia hayo mabadiliko!


   
 10. Thanda

  Thanda JF-Expert Member

  #10
  Sep 22, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 1,915
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kuna wasiojua na hawataki kujua kama hawajui
  Kuna wanaojua na hawataki kujua kama wanajua
  Kuna wasiojua kitu na hawajui kama hawajui
  Kuna wanaojua na wanajua kuwa wanajua
  Kuna wasiojua na hawataki kujua kama hawajui

  Sasa Kijakazi ajipambanue tena yuko wapi.
   
 11. Thanda

  Thanda JF-Expert Member

  #11
  Sep 22, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 1,915
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Tena Mungu anasema wanaositasita hapendezwi nao....Usipo mpendeza Mungu utampendeza shetani.
   
 12. Kijakazi

  Kijakazi JF-Expert Member

  #12
  Sep 22, 2012
  Joined: Jun 26, 2007
  Messages: 3,546
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 135
  Mimi nafikiri wewe ni Bw.Tendwa (msajili wa vyama) hautumii jina lako kamili au mna-share same genetic code!
   
 13. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #13
  Sep 22, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Yeah, Haukujua ? NAKULA PR na PESA za CCM...
   
 14. Kijakazi

  Kijakazi JF-Expert Member

  #14
  Sep 22, 2012
  Joined: Jun 26, 2007
  Messages: 3,546
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 135
  Tatizo ni kwamba sio kwamba sitaki mabadilko ila kusema kwamba sina hofu nitakuwa najidanganya nafsi yangu, kwa maana mifano iko wazi hapa Duniani ya watu wengi walioshangialia mabadiliko na sasa wanalia, kwa mfano Afrika Kusini wengi wao sasa hivi ukiongea nao wanadiriki hata kusema bora wakati wa Apartheid kulikuwa na Ubaguzi lakini walifanya kazi, hata Marekani kwenyewe wakati Bw. Obama anaapishwa watu mpaka walilia kwa furaha ya mabadiliko leo hii Takwimu zinasema 1 kati ya 5 waliolia na kumpigia kura Obama hawataki hata kumsikia, Misri walishinda Tahrir Square kutaka mabadiliko wakayapata leo hii baada ya Muslim Brotherhood kuingia, wanasema wangejua wasingeondoka pale Tahrir Square, hapo jirani Zambia juzi tu hapa walikuwa wanacheza barabarani kumshangilia Raisi mpya aliyeahidi kuondoa uonevu na wizi wa malighafi zao unaofanywa na Wachina leo hii hakuna jipya alilolifanya na Wazambia wanaendelea kupigwa Risasi na Wachina migodini, South Sudan walishangilia Uhuru toka Sudani kubwa leo hii hata chakula hawana na yule yule waliyemtangaza adui ndio wanarudi kumuomba chakula (Sudani kubwa), kwa hiyo mifano kama ndio inanipa hofu na sio kwamba sipendi mabadiliko ya wapinzani waingiwe ila nina hofu tu kidogo!
   
Loading...