pansophy
JF-Expert Member
- Nov 13, 2011
- 502
- 320
Kila nikiangalia kelele za wanao jiita wanaharakati pamoja na wanasiasa wa vyama vya upinzani wanavyohaha kuibuka na hoja mbalimbali ili kuongeza mitaji yao kisiasa wananikumbusha kipindi cha kwanza cha mechi ya fainali ilivyokuwa yakuvutia.
Benchi la ufundi lilifanya mabadiliko ya dharura kwa kumtoa yule mchezaji wetu mkongwe kwenye dimba la kati na kumuweka mchezaji machachari na mwenye uwezo mkubwa wa kugawa vyumba na kumudu dimba vizuri, mwenye kasi ya ajabu tuliye msajili kwa gharama kubwa 2015 na kumpa unahodha kwenye klabu yetu ya kinondoni iliyokuwa imesheheni wachezaji wenye vipaji kede kede na waliokuwa na usongo pamoja na molari ya juu wakipambwa na mashabiki waliokuwa na uchungu wa timu yao.
Timu ilianza vizuri, safu ya ushambuliaji na kiungo ilikuwa ipo vizuri sana. Nahodha mpya alikuwa yupo kila sehemu kuimarisha safu zote, alizunguka uwanja mzima bila ya kuchoka kwa hakika timu ilikuwa ipo vizuri. Pamoja na umahiri wote wa wachezaji na benchi la ufundi lililokuwa limesheheni wataalam kutoka nje ya nchi, dakika ya kumi na tano mabingwa watetezi walifanikiwa kuandika bao la kwanza lililopigwa kwa mkwaju mkali ndani ya boksi kufuatia shambulio lililopangwa vyema.
Bao hili limeitoa timu yetu kwenye mchezo kabisa, nahodha kashindwa kutuliza mihemuko ya wachezaji wake mpira umekuwa wa rafu nyingi, tumeelemewa kidogo, kelele na shangwe za mashabiki zimepungua sana. Nahodha amepata hitilafu kidogo anapatiwa matibabu na daktari kutoka tarime na hai, tunatumaini ataweza kuendelea na mchezo.
Kwako mwalimu Kashasha......