Kwa namna ulivyyomba huo ufadhili ni ngumu sana kueleweka kwani maelezo yamejibana sana pili ufadhili utatolewa baada ya kuona mwanzo fulani wa jambo lenyewe na hasa kukidhi vigezo vya kisheria kwa maana ya usajili wa biashara, utambulisho wa biashara mfano TFDA, TBS, BRELLA na kadhalika. Sasa ukiibuka kutokea hewani ndugu yangu sikukatishi tamaa lakini kimsingi unajikwamisha mwenyewe maelezo mafupi sana huwezi kuonekana kuwa serious hujataja umefanikiwa mpaka wapi umekwama kivipi na unategemea kurudisha vipi. Sio lazima utaje moja kwa moja lakini angalau mtu ajue kwa jumla jumla umefikia wapi na pili unategemea kuweka nini wewe mwenyewe na kuna guanrantee ya aina gani au bima gani ya kubeba biashara yako.
Kuomnba ufadhili kunahitaji weredi katika kupangilia hoja na kuziwakilisha ili ueleweke.