Nahitaji ushauri | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nahitaji ushauri

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Nacharo, Mar 9, 2011.

 1. N

  Nacharo Member

  #1
  Mar 9, 2011
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wandugu nina mtaji wa 5,000,000 hebu nishaurini nifanye biashara gani itakayonilipa.
   
 2. P

  Prime Dynamics JF-Expert Member

  #2
  Mar 9, 2011
  Joined: Dec 30, 2010
  Messages: 524
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Tafuta eneo kubwa la wazi, pata kibali manispa husika. Kuna watu wengi sana wanauza magari, au nyumba etc Kila mtu huwa anauza maliyake kwa sababu au shida alionayo mwenyewe. lakini madalali ndio wanao waangusha sana.
  Katika hilo eneo la wazi kila atakae taka kuuza gari lake atalileta hapo kwako siku ya juma mosi na juma pili pekee. (Siku mbili katika wiki). Utakua unawakutanisha mnunuzi na muuzaji moja kwa moja bila dalali.
  Kuhusu malipo yako weka kiingilio (5000 or 10,000) na fomu za kujaza. Kwa walio na nyumba za kuuza, watakuletea picha na bei zao. I'm sure you will end up making not less than 100,000 a day without investing more than 200,000. Badala ya watu kuweka matangazo kwenye magari "For Sale" watakua wanaleta kwako siku ya juma mosi na juma pili. Biashara hii itafaa only on weekends.
  Ukiletewa gari siku ya juma mosi, owner hana haja ya kusubiria hadi jioni, anaweza kuendelea na shuguli zake na akalirudia siku ya juma pili jioni. Hapo atakuta orodha ya contacts wanaotaka kufanya nae biashara.
  Advantage ya hii kazi ni kwamba muuzaji will have a better option of getting a person atakae nunua mali yake kwa bei poa.
  Jinsi ya kujitangaza. Sajili jina la kampuni yako, mafano HABARI Car Auction, print brochures weka contacts zako zisambaze. Sehumu ya kusambaza hizo brochures ni wakati wa traffic lights.

  Hii ni kama huna biashara unayo ifahamu kabisa.
   
 3. Mtanganyika

  Mtanganyika JF-Expert Member

  #3
  Mar 9, 2011
  Joined: Jul 18, 2007
  Messages: 1,613
  Likes Received: 280
  Trophy Points: 180
  Biashara nzuri ni kufanya kitu unachopenda... Jee unapenda vitu gani? weka hapa watu watachambua kimoja baada ya kingine
   
 4. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #4
  Mar 9, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Mkuu prime ina maana siku zingine za wiki kutakuwa hakuna magari?
  Huoni kama ni usumbufu mtu alete gari jmosi j2 alifate. Kama halijapata mteja wiki ijayo alipeleke tena?
  Na kuhusu kiingilio ina maana kila atakapopeleka gari itabidi alipie haijalishi gari itauzwa au la?
   
 5. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #5
  Mar 10, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Juu juu inaonekana biashara nzuri lakini angalia adha zake:
  1. Kuanzisha kampuni utahangaishwa na manispaa kupata kibali mpaka utakoma. Suala la rushwa litaingia hapo.
  2. Gharama za uandikishaji wa kampuni, ikiwa si kampuni bubu.
  3. Gharama za kukodi eneo inaweza kuwa kubwa kuliko unavyofikiria.
  4. Utahitaji ulinzi wa uhakika. mali za watu (mfano gari), ikiibiwa je?

  Ni mawazo yangu tu, kwa kuwa sijawahi kufanya biashara yoyote pengine yote haya hayapo.
   
 6. babalao

  babalao Forum Spammer

  #6
  Mar 10, 2011
  Joined: Mar 11, 2006
  Messages: 431
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mkuu kwani sasa kabla ya kupata huo mtaji ulikuwa unafanya nini na malengo yako yalikuwa yapi? Sidhani kwamba ulikuwa umekaatu tueleze tukushauri zaidi
   
 7. P

  Prime Dynamics JF-Expert Member

  #7
  Mar 10, 2011
  Joined: Dec 30, 2010
  Messages: 524
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35

  Mkuu hiyo biashara inafanyika only two days in a week yaani jumamosi na jumapili tu. siku nyingine za wiki hakuna biashara due to the fact that magari mengi yanayo uzwa na wenyewe wanayatumia kwa shughuli mbalimbali lakini kwa vile jumamosi na jumapili ni weekend, muhusika anaweka kuleta gari lake sokoni bila kumtumia dalali yeyote. Kuhusu kiingilio ni kila unapoleta gari unalipa due to the fact that muuzaji anarahisishiwa kupata mteja bila usumbufu mkubwa haijalishi gari itauzwa lini. Wanunuzi wa magari wataanzia kwako kabla hawaja enda kwingine. Hakuna usumbufu wa kuleta gari lako sokoni na kulirudisha nyumbani kwanza you may come up with a better idea unapokutana na wauzaji wenzio then you may end up exchanging vehicles according to needs of both parties.
   
 8. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #8
  Mar 10, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  nimekupata.
   
 9. P

  Prime Dynamics JF-Expert Member

  #9
  Mar 10, 2011
  Joined: Dec 30, 2010
  Messages: 524
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  1. Mkuu kweli kutakuwa na usumbufu fulani kupata kibali. Hapa muhusika should use his influence.
  2. Nivizuri kufungua kampuni since to deal with dead business hasara zake ni kubwa. Ili kuto'nekana tapeli nivyema kampuni iwepo.
  3. SIdhani kama utatakiwa kukodi eneo kwa sababu utogenga chochote katika eneo husika ila unweza kutumia tent kama mobile office. Pia demand ikiwa kubwa hapo utalazimika kujenga choo for public purpose which will be a credit kwa manispaa husika. Kinachoitajika ni kibali cha kupaki magari kwa siku mbili tu in a week.
  4. Ulinzi nilazima ila kuiba gari ni ngumu sana. Kwavile huwezi kuruhusu kutest gari kama muhusika au mwenye gari hayupo. You just need to be organized.
   
Loading...