Nahitaji ushauri wako na ni muhimu kwangu

Nahitaji ushauri wako na ni muhimu kwangu

Roho Mbaya

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2012
Posts
777
Reaction score
677
Mimi ni kijana wa miaka 26, Ni mtoto wa kwanza kwenye familia ya watoto sita kwa sasa najitegemea na nina kazi yangu

Wazazi wangu wote asili ya Mkoa wa Mara, Katika maisha yangu yote tangu mtoto nimekuwa nikimuogopa baba mzazi nahii ni kutoka kuwa mkali,vipigo vya mara kwa mara kwa watoto na hata wazazi wangu(mama na wake wengine wadogo wa baba mzazi). Ambapo hawa wake wadogo hawakuweza kuvumilia walikuwa wakiondoka nyumbani baada ya miezi kadhaa na hii ilikuwa inatokana na ukali wa mzee pamoja na vipigo, Kwangu mimi nimeshuhudia zaidi wake saba wakiondoka nyumbani na kuacha watoto.

Nakumbuka kwangu mimi mwenyewe kuchezea kichapo nilikuwa kidato cha nne, tulikuwa shambani tukilima kwa kutumia ng'ombe, ng'ombe waliacha mstari na kutoka nje kidogo mimi nilishitukizwa na mijaredi(fimbo zinazotengenezwa kwa ngozi ya ng'ombe)
Mpaka muda huu baada ya kumaliza masomo yangu na kuajiliwa lakini baba yangu mzazi bado hajabadilika-:
- ukorofi bado upo palepale
- Ugomvi na majirani
- Anazo kesi nyingi mahakamani
- Hataki ushauri kutoka kwa watu
- Ndugu wote wanamuogopa

Hivi sasa ana miaka zaidi ya hamsini lakini haoneshi mabadiliko

Ushauri wako nifanye nini ili abadilike
 
Wakati umebaki mdogo, Mzee wako Hawezi kukubali la mtu... mumvumilie hiyo ni hulka yake, sema ataacha taathira kubwa atakapo ondoka nyumbani, Wale wote waloondoka watarudi kuchukua haki zao!! wewe as elder son act wise.
 
Asante kwa majibu ila nachokushauri ndugu yangu hakuna unachoweza kufanya na kumbadilisha mzee wako, na sababu ni mfume dume wa watu wa ukanda wa musoma, na nakwambia hivyo kwa sababu mimi binafsi nimekaa huko musoma (kikazi) miaka 6; cha msingi ni kuwa wewe umeona mapungufu hayo kwa kuwa umekutana na wamakabila mengine na ukagundua hiyo si sawa, japo inawezekana ulianza kugundua wewe binafsi; cha msini kwa umri wa baba yako, amini huwezi kumrekebisha na wewe jitahidi kwa kuwa umeshajichanganya na tamaduni mbalimbali ni muda wako sasa kufanya tofauti na baba yako, ili na wanao waige mfano tofauti na wa babu yao!
 
Time will tell mkuu. Atabadilika tu bado kitambo kidogo umri utanyoosha muraas
 
Wakati umebaki mdogo, Mzee wako Hawezi kukubali la mtu... mumvumilie hiyo ni hulka yake, sema ataacha taathira kubwa atakapo ondoka nyumbani, Wale wote waloondoka watarudi kuchukua haki zao!! wewe as elder son act wise.

Hapo umenena
 
Mshauri apunguze kula kichuri na matumizi ya gongo!
vingne mwachie mama na Mungu!
 
Mpelekee mchungaji akamuombe ili usimwambie kama mmenda kumuombea,ila kuwa makini asije akawa"gecha"
 
Nakumbuka kwangu mimi mwenyewe kuchezea kichapo nilikuwa kidato cha nne, tulikuwa shambani tukilima kwa kutumia ng'ombe, ng'ombe waliacha mstari na kutoka nje kidogo mimi nilishitukizwa na mijaredi(fimbo zinazotengenezwa kwa ngozi ya ng'ombe)
I wish Mdingi wako ndio angekuwa MKUU wa nchi.
 
Back
Top Bottom