Nahitaji ushauri/msaada wa biashara ya karanga na masoko yake

Nahitaji ushauri/msaada wa biashara ya karanga na masoko yake

Mim nauliza je karanga za kusaga kwa matumizi ya kupikia zinauzika kwa mkoa wa tanga
 
Habari zenu wanajamvi natumaini ni wazima,

Samahani mimi nahitaji kujua na kupata ushauri pia kwa wazoefu wa biashara sana sana katika zao la karanga.

1.Njia nzuri ni ipi kwa mfano ukiwa na mtaji wa 5mil na ukaamua kulima karanga au ukiwa na mtaji wa 5mil na ukaamua kununua kusubiri wakulima wakime alafu kununua na kuifadhi na badae kuyauza?

2.Ni aina gani ya karanga ambazo ni nzuri na ambazo zina soko zuri?

3.Soko zuri la karanga?

Naomba kuwasilisha asanteni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wana JF naomba msaada wenu.
Ninafanya utafiti wa biashara ya kutengeneza siagi ya karanga. Nimerithi mashine ya kutengeneza peanut butter ila sina ujuzi wa soko hasa la Dar es Salaam. Mimi naishi hapa Dar.


Naomba mtu yeyote anayeujuzi wa hii biashara anisaidie kujua yafatayo;
1. Wapi nitapata Karanga zenye mafuta mengi
2. Bei ya Karanga
3.Wapi nitapata kopo za plastiki za ku-pack peanut butter
4. Bei la soko
5. suggestions za marketing


Natanguliza shukurani.

==========MASWALI MENGINE KUHUSU BIASHARA HII=====
Atupele tall ameuliza
Habari zenu wanajamvi natumaini ni wazima,
Samahani mimi nahitaji kujua na kupata ushauri pia kwa wazoefu wa biashara sana sana katika zao la karanga.

1.Njia nzuri ni ipi kwa mfano ukiwa na mtaji wa 5mil na ukaamua kulima karanga au ukiwa na mtaji wa 5mil na ukaamua kununua kusubiri wakulima wakime alafu kununua na kuifadhi na badae kuyauza?

2. Ni aina gani ya karanga ambazo ni nzuri na ambazo zina soko zuri?
3.Soko zuri la karanga?

================================================

MAJIBU YA WADAU KUHUSU BIASHARA HII
===============================================


Ni pm nikuonyeshe karanga ziliko na watu walio nazo au nenda katavi kijiji cha mwamapuli katafute kule bei ya gunia debe saba ni 36000

Sent using Jamii Forums mobile app
 
nikiwa kama kijana ninayependa kujituma, nimevutiwa sana na hii biashara ya kuuza Karanga. Lengo kubwa ni kutengeneza product yangu binafsi na kuweza kusambaza katika seehhemu mbalimbali.
Naimani humu ndani kuna wataalamu au watu wenye ujuzi mzuri wakuandaa Karanga na kuzikaanga vizur, hivyo ningependa kupewa mwanga hatua na namna ninavyoweza kukaanga karanga zikatoka bora na zenye ladha tamu...asante na natumaini nipata mrejesho mzuri kutoka kwenu
 
Natumaini mpo wazima wa afya njema ndugu zangu... pole na majukumu ya kujenga taifa letu...mimi ni kijana kati ya miaka 23 na 26 nina elimu ya form six (6)...ila kutokana na matatizo kidogo ya family sikuendelea na masomo maana ilikuwa nje ya uwezo wangu....Dhumuni\ lengo la uzi wangu ni kupata msaada\ushauri wa biashara ya karanga na masoko yake kwa dar es salaam na mikoa mingine...kuna binamu yangu ananipa milion 10 niifanyie biashara ya karanga, najua kuna faida na chagamoto zake kwenye hii biashara ya karanga.....natarajia mwakani mwezi wa tatu mwanzoni nitaanza kukusanya karanga nyekundu na nyeupe...kama kuna mtu/mfanya biashara wa zao hili la karanga na watu wengine wenye uzoefu na biashara za karanga naomba ushauri wenu kwa pamoja ili niweze kufanikisha malengo yangu ndugu zangu ..... nawasilisha.
Habari mkuu... Naomba kupata mwongozo wa soko kidogo kwa ulipofikia
 
1.Karanga nzuri ni zile nyeupe ndogondogo kama zinazopatikana Urambo-Tabora(Usinunue nyekundu).
2.Bei-Wakati wa msimu kuanzia April debe la maganda 4000/-(Kama una muda nunua za maganda ukoboe mwenyewe maana zina faida)
3.Vifungashio nafikikiri jaribu SIDO au makampuni ya plastics kama cello n.k(sina uhakika sana)
Mkuu kwa bei ya sasa itakuwa ni hiyo hiyo?
 
Back
Top Bottom