Nahitaji ushauri/msaada wa biashara ya karanga na masoko yake

Win

Member
Joined
Feb 3, 2012
Posts
33
Reaction score
13
Wana JF naomba msaada wenu.
Ninafanya utafiti wa biashara ya kutengeneza siagi ya karanga. Nimerithi mashine ya kutengeneza peanut butter ila sina ujuzi wa soko hasa la Dar es Salaam. Mimi naishi hapa Dar.

Naomba mtu yeyote anayeujuzi wa hii biashara anisaidie kujua yafatayo;
1. Wapi nitapata Karanga zenye mafuta mengi
2. Bei ya Karanga
3.Wapi nitapata kopo za plastiki za ku-pack peanut butter
4. Bei la soko
5. suggestions za marketing

Natanguliza shukurani.

==========MASWALI MENGINE KUHUSU BIASHARA HII=====
Atupele tall ameuliza
Habari zenu wanajamvi natumaini ni wazima,
Samahani mimi nahitaji kujua na kupata ushauri pia kwa wazoefu wa biashara sana sana katika zao la karanga.

1.Njia nzuri ni ipi kwa mfano ukiwa na mtaji wa 5mil na ukaamua kulima karanga au ukiwa na mtaji wa 5mil na ukaamua kununua kusubiri wakulima wakime alafu kununua na kuifadhi na badae kuyauza?

2. Ni aina gani ya karanga ambazo ni nzuri na ambazo zina soko zuri?
3.Soko zuri la karanga?

================================================

MAJIBU YA WADAU KUHUSU BIASHARA HII
===============================================

1.Karanga nzuri ni zile nyeupe ndogondogo kama zinazopatikana Urambo-Tabora(Usinunue nyekundu).
2.Bei-Wakati wa msimu kuanzia April debe la maganda 4000/-(Kama una muda nunua za maganda ukoboe mwenyewe maana zina faida)
3.Vifungashio nafikikiri jaribu SIDO au makampuni ya plastics kama cello n.k(sina uhakika sana)
 
I believe mpaka sasa biashara imesha anza.. tunaomba mrejesho mkuu, na majibu ya maswali yako..
 
Hapa Jamii forums mara nyingi huwezi kupata kitu. Inabidi tu mtu akomae kivyake. Watu wengi nyuzi kama hizi wanaziruka.
 
1.Karanga nzuri ni zile nyeupe ndogondogo kama zinazopatikana Urambo-Tabora(Usinunue nyekundu).
2.Bei-Wakati wa msimu kuanzia April debe la maganda 4000/-(Kama una muda nunua za maganda ukoboe mwenyewe maana zina faida)
3.Vifungashio nafikikiri jaribu SIDO au makampuni ya plastics kama cello n.k(sina uhakika sana)
 
1.Karanga nzuri ni zile nyeupe ndogondogo kama zinazopatikana Urambo-Tabora(Usinunue nyekundu).
2.Bei-Wakati wa msimu kuanzia April debe la maganda 4000/-(Kama una muda nunua za maganda ukoboe mwenyewe maana zina faida)
3.Vifungashio nafikikiri jaribu SIDO au makampuni ya plastics kama cello n.k(sina uhakika sana)

Vipi kuhusu machine? Zipo za aina gani na kwa bei ipi?
 
Wana JF naomba msaada wenu.
Ninafanya utafiti wa biashara ya kutengeneza siagi ya karanga. Nimerithi mashine ya kutengeneza peanut butter ila sina ujuzi wa soko hasa la Dar es Salaam. Mimi naishi hapa Dar.

Naomba mtu yeyote anayeujuzi wa hii biashara anisaidie kujua yafatayo;
1. Wapi nitapata Karanga zenye mafuta mengi
2. Bei ya Karanga
3.Wapi nitapata kopo za plastiki za ku-pack peanut butter
4. Bei la soko
5. suggestions za marketing

Natanguliza shukurani.

naomba uweze kuni pm ntakupa tech advice ya jambo hili kwa upana na urefu
 
Natumaini mpo wazima wa afya njema ndugu zangu... pole na majukumu ya kujenga taifa letu...mimi ni kijana kati ya miaka 23 na 26 nina elimu ya form six (6)...ila kutokana na matatizo kidogo ya family sikuendelea na masomo maana ilikuwa nje ya uwezo wangu....Dhumuni\ lengo la uzi wangu ni kupata msaada\ushauri wa biashara ya karanga na masoko yake kwa dar es salaam na mikoa mingine...kuna binamu yangu ananipa milion 10 niifanyie biashara ya karanga, najua kuna faida na chagamoto zake kwenye hii biashara ya karanga.....natarajia mwakani mwezi wa tatu mwanzoni nitaanza kukusanya karanga nyekundu na nyeupe...kama kuna mtu/mfanya biashara wa zao hili la karanga na watu wengine wenye uzoefu na biashara za karanga naomba ushauri wenu kwa pamoja ili niweze kufanikisha malengo yangu ndugu zangu ..... nawasilisha.
 
Kahama shinyanga kuna siko LA kalanga aise .ukifanikiwa uliza soko kuu kuna wateja sana hata kama utakuwa ma tani kumi ni fasta .0764505827 whatsap
 
Natumaini mpo wazima wa afya njema ndugu zangu... pole na majukumu ya kujenga taifa letu...mimi ni kijana kati ya miaka 23 na 26 nina elimu ya form six (6)...ila kutokana na matatizo kidogo ya family sikuendelea na masomo maana ilikuwa nje ya uwezo wangu....Dhumuni\ lengo la uzi wangu ni kupata msaada\ushauri wa biashara ya karanga na masoko yake kwa dar es salaam na mikoa mingine...kuna binamu yangu ananipa milion 10 niifanyie biashara ya karanga, najua kuna faida na chagamoto zake kwenye hii biashara ya karanga.....natarajia mwakani mwezi wa tatu mwanzoni nitaanza kukusanya karanga nyekundu na nyeupe...kama kuna mtu/mfanya biashara wa zao hili la karanga na watu wengine wenye uzoefu na biashara za karanga naomba ushauri wenu kwa pamoja ili niweze kufanikisha malengo yangu ndugu zangu ..... nawasilisha.
Kwa mtaji huo unaweza kuuza nje ya nchi pia na ukapata fedha ya kigeni. Kama utapenda kuuza nje ya nchi check na hii kampuni ya uwakala wa kununua au kuuza nje ya nchi www.kalumbilo.online unaweza kuwapigia hata kwa ushauri tu
 
lakini kuwa makini kuna watu wako macho hapa kuitazama hiyo 10m yako,so watakupa na contact ili wakuumizie huko
 
Kwa mtaji huo unaweza kuuza nje ya nchi pia na ukapata fedha ya kigeni. Kama utapenda kuuza nje ya nchi check na hii kampuni ya uwakala wa kununua au kuuza nje ya nchi www.kalumbilo.online unaweza kuwapigia hata kwa ushauri tu
Ahsante mkuu kwa ushauri.
 
Back
Top Bottom