ohio
Member
- Oct 29, 2020
- 55
- 128
Habari ndugu zangu, mimi ni kijana wa umri wa 25+. Niko hapa kuomba ushauri juu ya tabia yangu hii ambayo sasa naona imekua kero kwangu na kwa wanao nizunguka.
Turudi nyuma kidogo, katika utoto wangu nilikua mtoto mmoja mkimya na mpole sana, hakika nilipendwa na kila mtu mtaani kwetu. Baada ya miaka kadhaa nikaamishwa na wazazi na kupelekwa mkoa mwingine kwaajili ya masomo (nilikua darasa la nne), nilipofika katika ile shule nilianza kupendwa tena na kila mtu kuanzi walimu adi wanafunzi wenzangu hadi mtaani na nilikua mpole ila mtata sana.
Nilipofika sekondari (hapa ndipo nilipoanza kuijenga hii tabia) nilikua ni mtu wakujichanganya na watu ila sio mara zote na sio kila mtu kama ilivyokua shule ya msingi, huku nilikua nachagua watu wakuongea nao (nilikua najiona mtu fulani hivi ambaye sio kila mtu anaweza kuongea na mimi), ingawaje nilkua naongea na watu wengi.
Badae hii tabia ikahamia kwa wazazi nikawa sipigi simu nyumbani hadi niwe nashida ya pesa (hii tabia ikawa inamkela sana mama yangu ila hakuacha kunitumia pesa). Ilikua kama akituma pesa hadi hiishe ndipo anaona simu yangu (baba ndio kabisa hakuna hata sms sababu alikua hanisupport katika maswala yangu).
Nilipofika chuo huku ndipo ikakua zaidi nikafuta namba za watu wote niliosoma nao shule ya msingi hadi sekondari huku nikawa na washikaji wachache sana hawazidi 10, wapo ambao walitamani kua na ukaribu na mimi ila nikawa nawakwepa (wengine walinichana live kua naringa sana ila sikujali kitu). Marafiki zangu wakubwa walikua simu yangu na laptop, nilikua sipendi kukaa na watu wengi (yani kipindi kikiisha naondoka home sikua na muda wakupoteza chuo)
Kwa kipindi chote hicho hii tabia ilikuwa hadi kwa ndugu wengine na wale ambao tumezaliwa pamoja, kuna ndugu sijawasiliana nao miaka hata 10 inapita na namba zao ninazo na hata walikua wakinitafuta sipokei simu (nilikua sipendi kupokea simu zisizoingiza pesa). Hivyo sasa hivi hakuna ndugu niliye na ukaribu nae ukiacha wazazi tu.
Ukija mtaani, huu mtaa nimeishi kwa miaka 5 ila sijawahi kuongea na mtu yeyote.
Ukija kwenye mahusiano nimekua mtu wakuangalia makosa zaidi yani sidumu kwe mahusiano kwa muda mrefu kutoka na tabia zangu nimekua mtu wa kutoa amri na ifatwe na ubabe mwingi (mwanzoni nilikua naona sawa ila sasa ivi inanitesa). Kwasasa hivi niko kwenye mahusiano na mabinti fulani wawili ila uyu mmoja naona ameshakata tamaa, naona dalili zote za kupigwa chini (ingawa nampenda sana nilikua na mipango ya ndoa ila bidada kaona heri aachie ngazi) kwasababu ya gubu langu (anadai siko romantic) ugomvi kila siku, kutokujali na mazingira ya shughuli zetu yanatuweka pamoja kwahiyo najua vitu vyake vingi (naona kunajamaa anakwenda kuchukua nafasi yangu).
Kwakifupi nimekua na tabia yakujiangalia mimi tu . Naombeni ushauri ndugu zangu jinsi ya kuondoka na hii tabia ambayo binafsi inanikera na nmejaribu kuiacha nashindwa, hivyo ndugu zangu naombeni mnisaidie mbinu mbalimbali za kuweza kutengeneza tena mahusiano na ndugu zangu (sina ndugu yeyote ninae wasiliana nae kwa miaka zaidi ya 5 na hata kushiriki kwenye matukio ya kifamilia huwaga sishiriki niponipo tu). vilevile kuweza kutengeneza marafiki hatawachache (sina marafiki kwa sasa). Na kwanjia gani naweza kutengeneza mahusiano imara ya kimapenzi maana sasa hivi ninateseka sana na ninahitaji kubadilika. Napokea ushauri hata pm
SAMAHANINI KWA UANDISHI WANGU MBOVU ILA NAOMBENI MSAADA NAJIHISI MPWEKE SANA NAONA DUNIA SIO SEHEMU SALAMA TENA, NAONA NIPONIPO TU SINA FAIDA