Nahitaji ushauri katika kuibadili hii tabia

Acha kuvuta ganja Man ... ganja inakupoteza na ishakupoteza tiyari.... umeanza kuivuta Uko mdogo sana iache.
 
Kuna baadhi ya tabia hapo ambazo nilikuwa nazo kama wewe ila ukifikia umri fulani haihitaji ushauriwe ni namna tu ya kujiongoza mwenyewe


Mimi ni miongoni mwa watu waliokuwa hawaongei maneno ma3 kwa mtu yeyote hata mzazi nikikutana naye ni salamu na ishu nyingine basi, wakija wageni nasalimiana nao nikimaliza naondoka nakaa mwenyewe

Kilichonibadili ni chuo baada ya kupewa assignment ya kundi, nakumbuka nilikuwa mwenyekiti kundini, tukapanga muda wa kukutana kama saa kumi na mbili jioni, hakuna aliyetokea nikaondoka.... Imefika saa Tatu usiku wadau ndio wanakuja tukafanye kazi nikanyamaza kama kawaida yangu ila walipozidi kuzungumza nikawa mkali kwa kuwaropokea kuwa hawajali muda......

Asante Dr. Joseph popote ulipo, kuanzia hapo akawa ni mtu ambaye anakuja kunipigisha stori ili apotezee tukio lilotokea lakini nilipata matokeo chanya, yakuanza kujichanganya, stori za JF nazipeleka za uongo na ukweli ili mradi wa furahi nikajikuta napata chain ya marafiki ndugu na watu wengi kunikubali........

Kuna msemo amewahi kuniambia moja ya mashangazi zangu; MAISHA NI KUPANGA NA KUCHAGUA, HUKU WEWE UKIWA MPANGAJI AU MPANGUAJI YOTE UTAKAVYOONA WEWE

Katika hayo yote na umri ulio nao ilikubidi uanze kujiongeza kwa kubadilika mwenyewe, lakini ukiendelea kushupaza shingo, unaweza kukuta hata msiba umetokea au tatizo fulani au sherehe au kazi au chochote kile wataacha kukwambia kwasababu ya jeuri uliyo nayo



Yangu ni hayo kwa leo

Mr. Ben
Asante umenipa mwanga nitaanza kufanyia kazi
 
Aisee mimi hi tabia naipenda sana hata...kwenye simu...nina namba za watu muhimu tu pamoja na marafiki wachache sana....Lakini mimi kuna kitu kilisababisha hadi niwe kwenye tabia kama hiyo..
Mimi mwenyewe nilikua najiona niko sawa ila kwasasa hata hao watu wachache hawapo tena sio ndugu wala marafiki
 
Yani mkuu huna tofauti kabisa na Mimi,, nilidhani hii Tabia ninayo pekeyangu ..
 
saikolojia hiyo watu wa ujuzi huu watakusaidia lakini wachana na kujitenga
 
Sidhan kama pesa ndio utatuzi wa kila kitu
Pesa inatatua kila kitu..hata kifo inakirefusha

Nakuambia tafuta pesa hao ndugu utawakuta getini kila siku,nyumba yako itachangamka itakua na ndugu upande wa baba na mama,itakua na watoto wa wajomba na baba wadogo wanakuja kula sikuu kwa anko,itakua na wafanyakazi wa nje na ndani, utakua na chawa kibao wanakuja kunywa mnakaa garden mnacheza play station na kutizama mipiraa...niamini mimi
 
Binafsi hata mimi naipenda ila wengine sasa ndio wanapata shida sasa shida zao mimi hazinihusu maana huwezi nilazimisha niongee na wewe iwe unataka au hutaki,kama una jambo la msingi njoo ila kama huna wala siwezi kupoteza mda wangu
Hata mimi ni salamu afu miendo,nina marafiki wachache sana na vijiwe vichache saaana na bahati nzuri huwa napenda mpira tena kuangalia pekeyangu makelele na mabishano ya kwenye vibanda umiza naona kero sana.Uzuri wa hii tabia ni kwamba hutokuja kugombana na mtu popote pale si ofisini au nyumbani ila sasa uwe tayari kupitwa na fursa au matukio lakini pia jitahidi kujenga finanancial stability na kama ni shle uwe na uwezo hasa bila kutegemea wengine
Dah kumbe sipo mwenyewe, huwa nachukia kelele sana.
Au mishe za kugombana na watu sinaga.
 
Mabadiliko yanaanza na kubadili mawazo na mitazamo
Jifunze kuwa positive nakisia tu inaonekana hupendi kukwazwa ndomana unakosa ukaribu hadi kwa ndugu(migogoro haiepukiki mkiwa pamoja)
Jifunze kusamehe sio lazima kusahau ila tambua makosa ni udhaifu tu wa kibinadam
Pia jenga tabia ya kutoa misaada kwa wenye matatizo ya namna yoyote (hasa zile special group) na tembelea wagonjwa hospital wajulie hali na uwape moyo
Hayo yataondoa ubinafsi na kiburi
 
Kwanza nenda nyumbani, ongea na wazazi yako vizuri.. Muelezee kama ulivyo tueleza.. Wana mengi wata kwambia na yafuate...
Baada ya muda mpeleke mwenza wako kwenu na pia muende kwao..
Anza kuwa karibu na familia...
Nina imani tatizo litapungua au kuondoka...
 
😂😂
Maisha haya kuna wakati utafika nature itakubadilisha tu utake usitake.. nilikuwa na vijitabia kama vyako ingawa vyako vimenizidi..mpaka kuna muda Baba akawa anawaambia ndugu zangu wanidadisi nina shida gani..😂😂 dah!!

Ila umri unavyozidi songa taratibu unajikuta unabadilika na muda utafika utaiacha kabisa hiyo tabia.
 
Anza kwa kuwapenda jirani zako, wasalimie kila siku wajulie hali kisha wakumbuke wazazi wapigie simu hata mara2 kwa wiki.
Ila cha msingi anza na jirani yako kisha usambaze upendo
 
Utakuwa ulipata pigo Kali baada ya kumaliza sec


Pia pole sana nakushaurihuyo sim na laptop mtupe pembeni km ulivowatupa ndug jamaa na marafiki,,, kisha Fanya maisha kiuhalisia achana na maisha ya mtandao.
 
Umejitambua, sasa badilika! Ache kiburi na majivuno yako, jishushe. Anza kwenda kwa wazazi kukiwa na sikukuu, na uhudhurie shughuli za kifamilia ili ujiweke karibu na familia yako au hata marafiki.
Kikubwa acha kiburi na majivuno, utaendana na kila mtu.
 
Back
Top Bottom