Nahitaji TV LED 3D kuanzia nchi 32 na kuendelea

Nahitaji TV LED 3D kuanzia nchi 32 na kuendelea

ndugu yako

Senior Member
Joined
Mar 30, 2013
Posts
193
Reaction score
97
Wakuu kwema?!

Aisee natafuta TV LED 3D kuanzia nchi 32 na kuendelea iwe na miwani zake bei isizidi laki tano (500,000) nipo Dar,, mwenye nayo tuwasiliane kwa 0688 997179 au nichek pm.
 
Habari yako mkuu,
Niko china kwa sasa, natarajia kurudi tarehe 29 mwezi huu. Kama unaweza kukubaliana na mimi nitakuletea kwa 320USD full kit.
 
Kwa bei hiyo kama product ni quality nzuri ni rahisi sana,maana kuinunua,kuisafirisha na kuilipia kidogo kwa Tra ikiwa ni $320 ni cheap sana kwa 3D,Ndugu yako chukua mzigo huo.Hivi 3D Dvd ni tsh ngapi kwa Dar ??
 
kaka Godwin embu naomba model namba ya hiyo Samsung 3D 32' Tv ili niweze kui google nione sifa zake.
 
Achana na 3D tafuta 4K, kitu cha ukweli! 3D watu washaanza kusahau wewe ndo unatafuta, vuka hiyo stage nenda na 4K
 
kaka Godwin embu naomba model namba ya hiyo Samsung 3D 32' Tv ili niweze kui google nione sifa zake.

Samsung Full HD LED TV 3D
:81.28CM (32’’)
:Smart Motion Control F6400
:Resolution 1920X1080
:Series 6
:Support SD Card,Micro diming & USB
😛roduct Class is II (For abroad)
 
Achana na 3D tafuta 4K, kitu cha ukweli! 3D watu washaanza kusahau wewe ndo unatafuta, vuka hiyo stage nenda na 4K

Siku hizi ukitaka kununua kila toleo la tv/simu etc utachanganyikiwa maana kila siku mambo mapya yanaingia sokoni.Juzi nilikuwa sehemu moja wanapouza used mobiles nilishangaa kukuta Iphone 6 ikiwa kwenye maduka ya used mobiles !!!watu wengine wanasema hazifai japo ni toleo jipya!! sasa labda ungetuambia vitu vilivyopo kwenye 4K Tv ambavyo havipo kwenye 3D Tv ungekuwa umetusaidia sana.
 
Mkuu,
Hata mimi nimeona mdau hapo juu alichoandika. Pamoja na kwamba sijui kama aliwahi kufanya utafiti juu ya bidhaa aliyoeleza,niweke hapa mwanga kidogo japo kwa ufupi. Kampuni ya.Samsung (Wabunifu wa 2d, 3d na 4k), Kwa mara ya kwanza wameingiza sokoni TV Screens zenye uwezo huo wa 4k mwezi July 2014.
Screen walizoziingiza sokoni kwa kuanza na bei zao kwenye mabano ni Size 55’’ (US$2,500) Size 65’’ (US$4,000) na Size 78’’(US$6,500).
Tunatarajia huenda December wataweza kuachia hizo size za chini. Hata hivyo tusitarajie bei zake kuwa chini kiasi cha mtu wa mshahara wa kawaida kununua kirahisi,.
Huenda kuna kampuni nyingine zimetengeneza copy ya 4k flat screens lakini si kweli kwamba resolution inayoonekana kwenye TV ndiyo 4k. (Nimeziona baadhi hapa china)
 
4K ni tv zenye resulution kubwa mara kumi ya hizi HD zetu za sasa. Ili uifaidi hiyo 4k yako inabidi kuwe nakituo cha television kinachorusha matangazo kwa resolition hiyo, la sivyo utaendelea kupata resolution yetu ya kawaida kutokana na vituo vyetu vinavyotoa. Nasikia Japan kuna baadhi ya vituo vya tv vinarusha matangazo kwa 4k resolution
 
Achana na majina makubwa, ukitaka kununua bidhaa mpya nunua kampuni isiyokuwa na jina, hasa ukiagiza kutoka ASIA wanakuwa na majina mazuri na quality nzuri (bcoz zinakuwa zimetengenezwa kwa ajili ya soko lao) ila ukijua kuwa 4K TV lazima iwe Samsung lazima upigike ukinunua
 
Back
Top Bottom