Nahitaji partners kwenye kampuni yangu, je inaruhusiwa kisheria?

fredymkanza

JF-Expert Member
Jun 19, 2016
284
152
Heshima yenu wadau,

Naomba ushauri wenu nina kampuni yangu nilifungua mwaka jana ila mambo yanakuwa magumu sana, ni kipi napaswa kufanya?

Mpaka nimewaza kutafuta partiner ila sijui linakuwaje hili.

Ushauri wenu tafadhali
 
Elezea hiyo Company inajihusisha na nn na wapi umekwama pia huyo partner unataka kwa upande gani
 
Ok inajihusisha na cleaning service na car rental ila mwaka jana nimefanya marketing kwa gharama sana upande wa cleaning service na haijaleta matokeo kabisa
 
Kuna options 2; kwanza unaweza kumuuzia share huyo partner ili awe mmiliki wa kampuni kwa asilimia ndogo isiyozidi share zako ili mwisho wa mwaka mfaidike wote. Pili, kama na yeye ni kampuni/entity ya namna yoyote bhasi anaweza ingia mkataba wa partnership na kampuni yako kwa kutoa support yoyote ya kibiashara, e.g marketing costs, operational costs n.k au akatoa kiasi kadhaa cha pesa ili mwisho wa mwaka apate gawio la faida. ANGALIZO: kuna utofauti mkubwa kati ya 'shareholder' na 'partner'.
 
Back
Top Bottom