Nahitaji mshauri/ushauri

Nahitaji mshauri/ushauri

sojer

Member
Joined
Sep 4, 2018
Posts
71
Reaction score
47
Habari za majukumu wapendwa,
Nianze kwa kuomba radhi kwa baadhi ya watu kama nitakuwa nimewakosea kwa hiki nitakachoandika japo mimi naandika kutokana na yale nayopitia hivyo kama utanielewa nipo katika hali gani ushauri wako wa mawazo ni muhimu sana.

Kwa ufupi hapa nilipo kila jambo naloligusa kwa mikono yangu linafeli,kila biashara nayoanzisha inaanguka ,kila pesa nayoshika haifanyi chochote

Kwa sasa nipo dodoma nikiwa katika hali ileile ya kuzungukazunguka maana kwa sasa sina nyumba wala chumba nalala popote hasa kwenye vituo vya treni,nikipata hela mara mojamoja nalala guest,na mara nyingine nalala stendi za daladala

Yaani sina kambi maalumu na sina nyumbani wala ndugu kusema utakimbilia huko ukajishikiza huku ukiendelea kutafakali jinsi gani ufanye,

In short nipo katika mtihani ,ni rahisi kusoma haya nayoandika na kufikiria katika hali ya kawaida lakini hali yangu kisaikolojia haiko vizuri kabisa yaani rohoni naumia mno ila sina namna ya kufanya

Ushauri wako au mtu mwenye uwezo wa kunisaidia kibarua chochote chenye kambi utakuwa umenisaidia sana

Elimu yangu :ualimu (msingi) ngazi ya cheti hivyo kama kuna shule watahitaji mwalimu nipo tayari na niko vizuri

Umri : 25yrs
Jinsia :male

Kazi zingine kama zitapatikana nazoweza kufanya ni:
-kibarua cha kusaidia mafundi (hapa nimetafuta sana lakini napata za kusaidia za siku moja kesho hupati tena )hivyo nikipata ambayo ni endelevu hata mwezi itafaa zaidi
-na kazi nyingine yoyote ile naweza fanya
-

Kama utaweza kunisaidia kazi yoyote hapo juu nitashukuru zaidi

Ahsante

Pia ushauri wako unaweza niokoa
 
Mkuu maisha mapito ningekuwa na home ningelikuwa nimesharudi muda mrefu
 
Maelezo yako kwa mtu wa kawaida atakuona wewe ni mbabaishaji

Kusema huna ndugu na wala huna makazi (huku ukiwa na umesoma ualimu).

Mimi nimekuelewa, wewe hata ukipewa kazi utaendelea, "kutangatanga"

Kazi utafanya vizuri, ila baada ya muda utaona hapo kazini hapakutoshi (naandika hapa kwa uzoefu wangu na yaliyonipata hapo awali).

Msaada wa awali unaopaswa kupewa, upate sehemu ya kuishi (ukae hapo bure, kula, kulala n.k vyote iwe bure,)

Ikitokea umeondoka hapo, upewe nafasi ya kurudi pindi huko ulipokwenda mambo yatakapokwenda fyongo!

Hiyo itakufanya uwe unapata muda mzuri wa kupitia yote yaliyotokea hapo nyuma, na hapo ndipo utapata mwanga wa nini kinakupasa ufanye!

Ukijiingiza katika makanisa hapo umejipoteza.

Naandika kwa uzoefu siyo ubabaishaji!
 
Father of all Snipers,

Shukrani kiongozi

Nipo kwenye mtihani ambao kiukweli mbele naona giza tu

Kusoma ualimu bila ajira ni sawa na sifuri mkuu yaani hapa nilipo sioni chochote kinachoweza nisaidia kupitia huu ualimu zaidi ya kufundisha yaani katika maisha yangu naona hauna msaada wowote maana tangu 2015 nilipotoka chuo ajira hamna kabisa yani

Hivi najitahidi kupambana na vibarua lakini nikipata kamtaji nikianzisha biashara nikipata maradhi pesa yote huishia kwenye matibabu nikipona naanza na moja
 
Sasa,mkuu ,ukipewa kazi atakudhamini Nani? SI unajua uaminifu siku hizi ni tabu
 
Hufanyi kitu / biashara sahihi!
 
Sasa,mkuu ,ukipewa kazi atakudhamini Nani? SI unajua uaminifu siku hizi ni tabu
Mambo ya kudhaminiwa katika kazi nayaona ya kizee sana!
Wewe hujui hata matapeli / majambazi wanaweza kujipanga akapatikana muomba kazi, baba yake, mjomba wake mke wake n.k!
mpaka ukihitaji mwenyekiti wa kijiji analetwa.
Wewe kama unatoa kazi, mpe kazi,
Kama ni mwizi hata adhaminiwe na rais atakuibia tu.
 
Pole, naomba nikuulize maswali yafuatayo
1. Nyumbani ni wapi?
2. Wazazi au walezi unao?
3. Dodoma ulifikaje au ulipomaliza masomo uliishia mjini?
 
Nani kasema ntatumia udhamini huo unaoujua wewe!
 
Pole, naomba nikuulize maswali yafuatayo
1. Nyumbani ni wapi?
2. Wazazi au walezi unao?
3. Dodoma ulifikaje au ulipomaliza masomo uliishia mjini?
Mkuu walezi wapo ila hali yao ni ngumu sana na mara nyingi nikipata kiasi cha pesa huwa nawatumia hivyo nao ni tegemezi kwangu

Dodoma nina wiki now maana nilikuja labda kuomba udharula wa ajira wizarani lakini wamenitolea nje kuwa hamna kibali cha ajira now
 
Anza kuuza smartphone kwanza, kabla ya hapo acha mbu wakutafune kwanza ili ujue hata Nokia ya tochi inafaa kwa mawasiliano pia
 
Anza kuuza smartphone kwanza, kabla ya hapo acha mbu wakutafune kwanza ili ujue hata Nokia ya tochi inafaa kwa mawasiliano pia
Mkuu nimeuza vitu vingi sana vya ndani na nilivyokuwa navyo hivyo kuuza simu sioni kama itakuwa solution na mara nyingi simu kama inanisaidia kutoa stress nikiingia mtandaoni na vitu kama hivyo na kwa asilimia kubwa simu ndo inanisaidia sana na nikiuza ndo naona maisha yatakuwa mabaya sana mkuu nilijaribu kuwaza hivyo lakini naona effect ya kuuza simu na kukaa bila simu ni kubwa sana
 
Weka namba yako ya simu hapa ili nikuhoji vizuri kwanza
 
  • Thanks
Reactions: amu
Yote yatapita mkuu,ni nyakati tu tunazopitia. Tambua kuwa huwezi kubaki hivyo milele.
 
Back
Top Bottom