Nahitaji msaada wenu

Dirham

JF-Expert Member
Dec 26, 2016
491
536
Naanza kwa kumshukuru Mungu kwa kutupa uzima na afya njema mpka wakati huu. Pili napenda kutoa salam zangu zikufikie wewe unaesoma thread hii popote pale ulipo na mungu akubariki sana.

Mimi ni kijana na nina familia ya mke na watoto wawili. Nimshukuru mungu baada ya kumaliza elimu yangu ya chuo ngazi ya shahada ya kwanza nilipata kazi mkoan Tanga maisha yakaendelea, niliweza kukidhi haja mbalimbali za familia yangu na kuendesha maisha. Baada ya mwaka mmoja wa kazi nilianza kupatwa na hali ya ajabu sana, kwanza kuwa na usingizi mzito sana asubuhi pili kutokuwa na morali ya kazi.

Kwa muda mrefu sana nipipigana na hii hali ambayo ilipelekea kutokuwa na ufanisi mzuri katika utendaji kazi. Nilijaribu kutafuta ushauri kila mtu alisema lake nilojikaza na hatimae miaka miwili ikapita lakini katika hali ngumu sana pesa haikai na niseme tu mimi sina matumizi mabaya ya pesa halafu si mtu wa anasa.

Nikajikuta naingia kwenye madeni ambayo yalipelekea mshahara wangu kupinguwa sana na hata kufikia hatua mshahara hautoshi hali ilikuwa ni mbaya sana. Ni muda mrefu sana nimekuwa mtu wa kutopata usingizi usiku, nilipambana kwa hali zote lakini haikiwa riziki yangu nikasimamishwa hivyo nikarudi nyumbani.

Nimejitahidi kutafuta kazi lakini nimekosa ilifikia point nikaona bora nijiue lakini nikifikiria wanangu na mama yao wananitegemea. Inabidi nipambane kwa ajili yao sina kazi ikabidi nianze kudeal na vibarua nipate 2000 watoto wangu wale. Ni maosha magumu sana haya najua ni mitihani nami sikati tamaa.

Lengo la kuandika historia fupi ya nilikopitia mpaka hapa nilipo sasa ni kutaka msaada wenu wana JF

1. Tangu mwanzo wa hii wiki imekuwa ngumu sana kupata vibarua imepelekea ugumu sana kupata chakula. Nina watoto wawili wadogo mkubwa ana miaka 5 na mdogo ana miaka 3 naumia sana roho ina niuma sana nikiwaona nashindwa kuwapa milo yote mitatu. Jana usiku wamelalia uji na leo asubuhi nimeondoka sijaacha kitu kwani hata senti sina. Ndugu zangu kwa mwenye uwezo wa kunistiri familia yangu leo ipate chakula nitashukuru sana.

NB.:Nakushukuru kwa kusoma thread yangu na mungu akubariki sana na uwe na siku njema.

Amiin
Kwa alie teyari kunipa msaada wa aina yoyote naomba tuwasiliane PM
 
Mkuu, uliwahi kujihusisha na kamari kwa muda mrefu...??
Hapana mkuu ila kuna kipindi nilijaribu kufanya michezo ya kubahatisha nikiexpect kuongeza kipato lakini nako nilifail sikuendelea nako tena
 
Naanza kwa kumshukuru Mungu kwa kutupa uzima na afya njema mpka wakati huu. Pili napenda kutoa salam zangu zikufikie wewe unaesoma thread hii popote pale ulipo na mungu akubariki sana.

Mimi ni kijana na nina familia ya mke na watoto wawili. Nimshukuru mungu baada ya kumaliza elimu yangu ya chuo ngazi ya shahada ya kwanza nilipata kazi mkoan Tanga maisha yakaendelea, niliweza kukidhi haja mbalimbali za familia yangu na kuendesha maisha. Baada ya mwaka mmoja wa kazi nilianza kupatwa na hali ya ajabu sana, kwanza kuwa na usingizi mzito sana asubuhi pili kutokuwa na morali ya kazi.

Kwa muda mrefu sana nipipigana na hii hali ambayo ilipelekea kutokuwa na ufanisi mzuri katika utendaji kazi. Nilijaribu kutafuta ushauri kila mtu alisema lake nilojikaza na hatimae miaka miwili ikapita lakini katika hali ngumu sana pesa haikai na niseme tu mimi sina matumizi mabaya ya pesa halafu si mtu wa anasa.

Nikajikuta naingia kwenye madeni ambayo yalipelekea mshahara wangu kupinguwa sana na hata kufikia hatua mshahara hautoshi hali ilikuwa ni mbaya sana. Ni muda mrefu sana nimekuwa mtu wa kutopata usingizi usiku, nilipambana kwa hali zote lakini haikiwa riziki yangu nikasimamishwa hivyo nikarudi nyumbani.

Nimejitahidi kutafuta kazi lakini nimekosa ilifikia point nikaona bora nijiue lakini nikifikiria wanangu na mama yao wananitegemea. Inabidi nipambane kwa ajili yao sina kazi ikabidi nianze kudeal na vibarua nipate 2000 watoto wangu wale. Ni maosha magumu sana haya najua ni mitihani nami sikati tamaa.

Lengo la kuandika historia fupi ya nilikopitia mpaka hapa nilipo sasa ni kutaka msaada wenu katika mambo haya mawili wana JF.

1. Tangu mwanzo wa hii wiki imekuwa ngumu sana kupata vibarua imepelekea ugumu sana kupata chakula. Nina watoto wawili wadogo mkubwa ana miaka 5 na mdogo ana miaka 3 naumia sana roho ina niuma sana nikiwaona nashindwa kuwapa milo yote mitatu. Jana usiku wamelalia uji na leo asubuhi nimeondoka sijaacha kitu kwani hata senti sina. Ndugu zangu kwa mwenye uwezo wa kunistiri familia yangu leo ipate chakula nitashukuru sana.

2. Kwa yoyote ambae anaweza kunipa kazi ama kunipa connection yoyote ya mimi kupata kazi nitashukuru sana. Nahitaji kazi ili niendeshe famipia yangu vizuri, sijiwazii mimi bali niwazia na kuifikiria familia yangu kwani mimi ndie baba na wananitegemea wanangu bado wadogo sana.

NB.:Nakushukuru kwa kusoma thread yangu na mungu akubariki sana na uwe na siku njema.

Amiin
Kwa alie teyari kunipa msaada wa aina yoyote naomba tuwasiliane PM
Sasa mkuu unataka connection wakati hujaweka fani ya ulichosomea, vipi tatzo lako la kusinzia ulishalitafutia ufumbuzi na ukajua chanzo chake?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapana mkuu ila kuna kipindi nilijaribu kufanya michezo ya kubahatisha nikiexpect kuongeza kipato lakini nako nilifail sikuendelea nako tena
Sawa mkuu, maana hadi nimeuliza hilo ujue kuna jambo nimelifuatilia kwa kina kukuhusu.
By the way, pole kwa magumu na changamoto zenye unapitia.
 
Sasa mkuu unataka connection wakati hujaweka fani ya ulichosomea, vipi tatzo lako la kusinzia ulishalitafutia ufumbuzi na ukajua chanzo chake?

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu suala la usingizi mpaka sasa bado linaendelea kulala kwangu saa 7 ama 8 ni vigumu sana kupata usingizi mapema. Mkuu ufumbuzi bado sijapata mpaka sasa nahangaika na kula ya wanangu
 
Back
Top Bottom