Habari wana jamii wenzangu. Nimeolewa, kabla sijapatwa na mkasa ninaotaka kuwaeleza nilikuwa namuamini sana mume wangu. Mwaka jana mwezi wa 6 nikagundua kuwa ana mwanamke (mama mtu mzima ) Kuanzia hapo moyo wangu umekuwa mgumu sana kumwamini ingawaje tulishayaongea na alikiri na kuniomba sana msamaha ila kuna wakati kumbukumbu zinanijia na ghafla najikuta namchukia mno. Niasaidieni cha kufanya coz nahisi nimeathiriwa na tukio kwa kiasi kikubwa sana. Imefikia mahali sifurahii tena tendo la ndoa na kuna wakati naweza kumnyima hata mwezi mzima. Kabla ilikuwa tunashirikiana vizuri tu ila kwa sasa nipo nipo tu. Huwa najiuliza je kama niliweza kumtimizia kila kitu kama mume na bado akanisaliti kwa nini niendelee wakati nmeshagundua kuwa hatosheki? Kweli naishi nae basi tu ila moyoni kwangu hayupo kabisa. Nilishamwomba tuachane kwa upendo akakataa eti tutamwathiri mtoto, eti bado ananipenda ni shetani tu alimpitia na hatampitia tena. Anachonikera zaidi ameanzisha tabia ya kunichunga kama mbuzi, hata nikienda saluni siondoki mpaka aje kunichukua, madai yake eti anaogopa nitamlipizia. Nikiwa kazini cm masaa yote na anafika kunichukua dakika 5 kabla ya muda wa kazi kuisha. Nisaidieni wajameni coz kweli sina upendo na huyu mtu. Hilo jimama alishaliacha na viapo tele kuwa hatarudia tena. MOYO MGUMU KUSAMEHE! NIFANYEJE???
Sweety pole sana. Hebu jaribu kufikiria kama wewe shetani amekuningilia ukammgea X wako au class mate wako enzi hizo mkicheza cheza.
Halafu huoni jamaa yako ni mwungwana sana ? Sisi wanaume hatukubali kama tumemega hata kama umeshikwa live . Huyo wa kwako ni exception otherwise inawezekana kakudanyanga ili upate wivu zaidi. Anakufuata kazini, cm kibao, saloon darling ,darling......... halafu unaona kinyaa? Anakupenda, to put story very short.
Muhimu hapo ni kuokoa ndoa yenu.
Tumia nguvu zako zote na busara zako zote umsamehe, yaishe, halafu rejesha mapenzi yako kwake, zidisha kuliko zamani. Yaani hapo, ni kwamba unamdhibiti kwa kumwonyesha mapenzi zaidi badala ya kumchunga au kumchunguza (si ajabu kumchunguza kwako ndiko kulikopelekea maumivu ya kufahamu ukweli). Pia ni vizuri ukatathmini sana ni kitu gani kilipelekea yeye kuanza kutembea nje.
Kupunguza mapenzi na hisia zako kwake, hakuna tija kabisa, kunapelekea yeye kuzidi kujishuku na kukosa amani na baadaye anaweza kuendelea kulamba nje tena.
It appears na wewe una jamaa nje ndo maana unamuona anakughasi kwa kukupeleka saloon etc na kukupigia cmu. Maana si bure. Kama ni msamaha amekuomba, anakufata office on time, saloon anakupeleka etc. What do caring and love mean to you. Mwisho wa siku What do women want after all those carings/love from your lovely ones? To me it sounds huyo jamaa amejirudi sana, and that means kama alikua anachelewa nyumbani sasa hv mnaenda wote. Mnataka nini nyie wanawake? Mkipendwa kosa, mkitukosea - tukateleza na cheat nje kosa.......
Aksante ndugu yangu, ni kweli baada ya kumgundua aliniweka wazi kila kitu mpaka mara ngapi ameduu na huyo mama ila kinachonifanya niwe mgumu kumsamehe ni kwamba by the time nagundua uhusiano wao huyo mama alikuwa na mtoto mchanga nikamwuliza na mtoto ni wako? Akajibu ndiyo, ila hana uhakika coz mama mwenyewe yupo single na anamegwa na kila mtu. nikamwambia sasa kwa nini unasema mtoto ni wako akajib eti jimama ndo linemiambia ni wangu. HAPO NDO AKANIWUWA KABISA!!! KUMBE HATA SEX ALIYOFANYA SI SALAMA KIASI HICHO? AKADAI ETI SIKUTUMIA KINGA MARA MOJA TU? SASA HEBU NIAMBIE KAMA NI WEWE UNGEMWELEWAJE??
Pole mumie nipigie nikupe ushauri zaid na kukupunguzia mawazo.
NI ngumu kweli . Ukimwacha atahamia kwa jimama na ndio mwisho wa hii stori. Bila shaka utaumia zaidi ukimkuta ndio baba watoto kadhaa wa jimama. La msingi ni kusamehe yaishe mjenge familia.
pole sana mpz,kujikwaa si kuanguka,najua kuna wengi sana wanacheat na hawakubali kosa,tena unaweza kuwakuta red handed bado akasema"it wasnt me"kama umeamua kusamehe basi samehe na kusahau kabisa maana kama hujasahau huo ni unafki tena unapata dhambi(am not judging)unapomnyima unampa ham ya kurudi nyuma,songa mbele dada,fanya jema na wajibu wako kama mwanamke Mungu atakulipia uliapa kwa shida na raha so its beta ukashinda majaribu,lkn mwambie Mungu shida zako maana yy ndie aliemuumba,muombe amfinyange upya na kumrekebisha.