Nahitaji msaada wa kusonga mbele

Nahitaji msaada wa kusonga mbele

Aisee!!!!! nakuonea huruma sana.

Hebu jifanye unajipenda wewe kwanza sio mtu mwingine, kisha tuliza akili na omba upate mwingine atakayekufaa.
 
Tema mate kushoto ufukie kuliaaaa maisha yasonge mbele.....
 
angelita

huu ndio ule wakati muafaka wa kutumia AKILI badala ya HISIA.....
 
Last edited by a moderator:
DUNIA ni sehemu yenye kupendeza na kufurahisha ikiwa tu utachagua kuishi kuenenda na hali halisi na si kwa matakwa ya msukumo wa nafsi yako...mapenzi ni sehemu ndogo ya maisha yetu ya kila siku lakini mapenzi peke yake hayakimilishi maisha yetu...

.Mioyo yetu inapoanguka penzini hutuvika upofu hata tusione upande mwingine wa furaha katika maisha yetu...hutufanya tuwe watumwa ndani ya fikra zetu wenyewe kiasi cha mtu kuamini hawezi kuishi bila ya uwepo wa mtu Fulani hapa duniani.

..Lakini haya mateso huwatokea wale wote waliochagua mihemko yao kuwa ndio dira zao ziongozayo maisha yao...na wanaokataa kuishi kulingana na hali halisi ya mazingira yaliyopo sasa...Tiba pekee ni kuukubali ukweli na kuishi kuenenda na ukweli huo...na hapo ndio utakapoona dunia ikiwa kama PARADISO yenye kuvutia na kupendeza...

We jamaaaa....unamtizamo chanya sana....Nataman watu wote, tuwena perspective hiii
 
Ata me mwenyewe ni miaka 4 sasa nmeshindwa kukutoa moyoni turudiane tu
 
angelita pole mydia, kudate mume wa mtu ndio uliongeza mateso yako kwa sababu ulimuharibia mwanamke mwenzio ndoa yake na ndio maana nafsi yako inajuta.

Tulia, relax then tafakari maisha yako upya then Februari mwakani utakuja kutangaza furaha yako hapa.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom