Mpenzi, kwakua umesema upo dodoma hebu anzia hospital mirembe kwanza kwa madaktari wa magonjwa ya akili then ikishindikana tafuta msaada wa kiroho kama ulivyosema, siku hizi watu wengi wanaugua magonjwa ya akili bila wao kujitambua. Nenda kajaribu masuala ya kitabibu kwanza, Uzuri Doctors wanaoamini Mungu huwa wakiona kitu ambacho sio kawaida huwaambia ndugu wa mgonjwa ili wakajaribu mambo ya rohoni.
Ikiashindikana huko, i recommend you uende kanisa moja lipo maeneo ya Area A, near Matovolwa hosp, ukutane na mchungaji E. Manwele mueleze shida zako zote na historia yote atakupa huduma, mtaanza kwa kufunga hata kwa wiki na maombi mazito, Mungu atakufungua kutoka katika vifungo. Speaking of wachungaji, mchungaji wakweli haponyi, humsaidia kondoo wake kukua kiimani, kumjua Mungu zaidi, humfundisha neno na kumuelekeza kuenenda katika neno, kupitia haya ndipo uponyaji hupatikana, naye Mchungaji kwa kuwa ni mpakwa mafuta wa bwana basi huwa na kibali chakufikisha maombi ya kondoo wake wa Mungu. Ogopa wale wanajisifia miujiza na kuponya, na hasa katika kipindi hiki punguza kuwa desperate, Be careful na makanisa mengi unayoambiwa uende utapoteza pesa na muda mwingi maana huduma hii siku hizi imejaa makanjanja. Ila nakuomba sana ndugu anzia hospitali, All the best.