Habari za humu ndani?
samahani kwa nitayemuudhi labda kwa kuweka wazi sana maisha yangu, ila waswahili husema mficha uchi hazai na mficha maradhi kifo humuumbua! Najua humu ndani kuna watu wakubwa,wenye nyazifa tofauti,matajiri wenye uwezo tofauti,wafanya biashara, watu wenye fani tofauti n.k .
Naomba mnisikilize nakuja mbele yenu ninaomba msaada wenu na natumahi kuwa ipo siku ambayo haina tarehe wala saa nitarudisha fadhira kwa atakayenitoa katika shimo hili.
Mimi ninakaa Dar es salaam, katika kipindi cha kusoma kwangu nimejitahidi kukusanya hela kiasi japo kwa shida sana sana ili zije zinisaidie baadae! nilivomaliza ikabidi sasa nianze kutumia hizo hela katika kujitegemea na kutafuta maisha kiujumla! nikawaza nifanye biashara gani ambayo ni risk calculated business! nikaona afadhari biashara ya juice kwa kuzingatia hali ya jiji hili la Dar!
Basi kiasi fulani cha hela nikanunua freezer, brender na juice dispenser pamoja na nikatengeneza baiskeli maalumu itakohusika na usambazaji wa juice! kwa kuwa ndo kipindi cha joto kinaanza sasa nikawa natakiwa nianze kazi rasmi!
MTIHANI SASA
hizo hela nilizojitahidi kuzikusanya kwa shida sana sasa zimeisha kutokana na kwamba nimenunulia hivyo vifaa na pia kwa matumizi binafsi ukizingatia hamna mtu ninae mtegemea anipe hela ya matumizi!
Mzazi wangu nashindwa kumuomba maana yeye sasa hivi ana mitihani saa nyingine nikimsikiliza japo kwenye simu nataman hata kulia!! Sasa kwa sasa sina hata hela ya kula, nimekuwa mtu wa kuomba omba ili mradi tu nipate ya kula, ndani sina kitanda wala godoro nimelalia chini kwenye sakafu mpaka sasa najiuliza kwa nini mimi??
Kodi inakaribia kuisha nina karibia mwezi mmoja hivi kodi kuisha pia ninahitaji hela ya kulipia kwa mwezi kama umeme,maji na usafi n.k !! tangia nianze kusoma sijawahi kupata raha maana kila siku imekuwa ni mitihani tu!! nimemaliza chuo bado ni mitihani tu na naona inazidi!!
Nimesoma chuo bila mkopo na kushinda njaa ni kitu ambacho ni utaratibu wa kila siku ila kwa sasa mpaka inafikia hatua sijui kesho yake nitakula nini!!! Mtu unaweza kujiuliza kwamba kwa nini nisitafute kazi??? kazi zinataka ujuane na watu na pia kazi siwezi kuipata sasa hivi na nilipwe sasa hivi ukizingatia sasa hivi sina hata cheti!
Pia kuhusu kufanya kazi hata za kutwa nipate hela ya kula imekuwa ngumu kutokana na kwamba kila siku nimekuwa mtu wa kuzunguka kutafuta jinsi ya kutatua matatizo haya! kwa hiyo mpaka nikaona siwezi kupata mda wa kufanya kazi hata itakayonipatia elfu tano kwa siku!!
Nimehangaika sana kutafuta mtaji wa kuendeleza hii biashara yangu ila nimekitana na mitihani mingine zaidi maana sina nyumba wala ardhi wala leseni ili kuweka kama dhamana pia hata watu wanaotoa kwa riba nao wana masharti magumu sana ukizingatia sina kitu cha thamani zaidi kuweka kama bond!! Nimetafuta kwa ndugu,jamaa na marafiki ila kila mtu ananiambia hana hana kabisa mpaka ninabaki nikiwa sina jinsi ya kufanya nikaona nije hapa ili kuona kama kuna mtu ataweza kunisaidia katika hili!!
Mimi binafsi nimesomea biashara na ninapenda biashara! napenda sana ujasiriamali na nina ndoto kubwa sana za kutoka kimaisha na kuwa successful person hapo baadae!! Nina amini katika kupambana zaidi na nina penda kuchakalika huku na huku kufanya biashara! Pia nina uzoefu na kazi na hotel, mambo ya juice n.k
NINACHOHITAJI
Naomba mtu ambae anatamani na ana uwezo wa kunisaidia anisaidie maana nipo katika kipindi kigumu zaidi katika maisha! ninaomba mtu anikopeshe laki sita tu ili niweze kulipia kodi pamoja na kumalizia mradi wangu! kiasi nimeamua kulipia kodi kwa sababu vifaa vya kutumika katika uzalishaji ninavyo kama freezer, brender na juice dispenser ila ni marekebisho kidogo tu yanahitajika kuongezewa kwenye juice dispenser na hiyo baiskeli maalum niliyotengeneza!!! Kwa hiyo niko serious na hela hizi!!!
Ninaomba hata kama mtu akitaka kunikopesha kwa riba na tukaandikiana niko tiyari na akitaka niweke bondi vitu vyangu ntaomba vitu niendelee kuwa navyo maana ndivyo nitakavyokuwa natumia katika uzarishaji!!! Ila hata kama mtu atataka kujitolea kama msaada tu napenyewe nitashukuru sana maana na Mungu nae atamuongezea zaidi!
Usiwe na wasiwasi labda hela nitairudisha vipi ni kwamba nikipata hicho kiasi nitarekebisha juice dispenser yangu na nitaiweka sehemu penye watu wengi nina imani nitauza tu na ukizingatia juice ina faida tu nzuri na pia kwa hapa Dar es salaam itaenda vizuri. Pia kwa kutumia hiyo baiskeli nitamuweka kijana ambaye atasambaza mjini ili niwe na uhakika hela inarudi haraka sana! hata hivyo kwa kutumia freezer yangu naweza kuongeza biashara nyingine kama maziwa mtindi , ice cream,maji n.k! nima imani hela nitaweza kuirudisha!
Binafsi nilitamani milioni moja ili angalau nipate hata hela ya kununulia godoro au kitanda cha kawaida sana maana inaumiza sana kulala chini kwa mda mrefu! lakini kwa yeyote mwenye uwezo nitashukuru sana akinisaidia hiyo laki sita au akiweza hata milioni moja tu!
MATEGEMEO YANGU
Kama nikibahatika kwa siku nikatengeneza 20,000 haya yakiwa ni makadirio ya chini zaidi ina maana kwa mwezi nitapata laki sita! na pia kumbuka faida inaweza kuongezeka zaidi hata kufikia 40,000 na zaidi! kwa maana hiyo nitaweza kurejesha mkopo huo baada ya mda furani!
Naomba mtu mwenye uwezo aniamini maana naelewa hii ni pesa pia naelewa hichi ni kipindi kigumu sana pesa haipatikani kirahisi! lakin hata hivyo ntaomba mtu huyo aniamini sana maana nina uchungu sana na maisha !!!! pia mimi sio mtu wa starehe sinywi pombe,sivuti sigara,naishi mwenywe na sina mke wala mtoto! naomba msaada wenu tafadhari.
Atakayehitaji aniandikie sms DM ili tuweze kuwasiliana zaidi!