Nahitaji msaada wa haraka kabla stress haijapanga chumba moyoni mwangu

Asante mkuu
 
Imeandikwa "Samehe 7x70". Samehe kisha sahau.
Kumbuka haijaandikwa ombwa msamaha ili usamehe.
Lengo ni kuwa usiposamehe wewe unadhurika wakati mtesi wako anafurahia kukukera.
 
Huwa nikishamgundua mtu ni mkorofi or anatabia siyo nzuri na ananikela, kwa vyovyote nitaanza kujitenga nae. Na kama nikikutana nae ni salamu tu basi baadabya hapo nakuwa kimya.
 
Pole sana, itabidi ujifunze kusamehe, tena kuanzia sasa, sababu wewe mwenyewe naamini unawakosea watu, twaamini wewe pia hujakamilika, twaamini wewe siyo malaika, kwa point hizo dada anza kusamehe kuanzia sasa, ama sivyo kinyongo na hasira zitakuuwa kabla ya wakati wako..Pole sana
 
hhakuna njia nyingine zaidi ya kuamua wewe mwenyewe kutoka moyo.hata hatua ya kuamua kuandika hapa maana yake unaanza kupona.
 

unamshauri au una mpoteza.
 
Ukishasamehe

Achilia

Kisha

Jiepushe nao


Mwisho


Dharau makwazo yao...yaani waone kama wapuuzi fulani tu

Na ukiwa kama mie.....

Nakupa za uso kwanzaaaaaaaa nikitoka hapo mwepesiiiiiiii
 
Nimesoma bandiko lako na kugundua haya machache;
i).Hujui kukataa pale mtu anapokuomba kitu au jambo fulani
ii).Hupendi kumuudhi mtu
iii).Furaha yako unaiminya
iv).Kuna ndoto (neno zuri hapa ni expectations) ambazo umeweka juu ya mtu au watu unaoishi nao wanaweza kuwa marafiki, wafanyakazi, majirani na hata ndugu pia. Hapa pia naweza kuongeza suala la uaminifu bila kujiridhisha katika mda mfupi wa kujuana.
V). Ni mtu wa kujipendekeza kwa watu waliokuzidi kifedha au kimaisha.

♢Suluhisho ni kuishi tafauti na hizo assumptions hapo juu.♢

Sijui umri wako lakini unaweza kuwa ni millenial hivyo basi kama ni mapenzi yape kisogo jenga maisha kwanza. Usikubali kutumika na mtu kisa ana jina, fedha au uzuri/utanashati. Pia usiwe king'ang'anizi ukiamini ipo siku atabadilika au mambo yatakuwa sawa.
 
Umejibiwa vyema, ukifanyia kazi shauri hapo juu utapona.
Nami niongeze kidogo.
Ili uweze kusamehe basi acha kujiona wewe victim. Una mchango mkubwa ktk kile unachofanyiwa na unahusika pekee ktk the way una react. Maelezo mengi juu yamejikita ktk the way unavyoreact. Mimi ningependa ujifanyie tathmini ya mimi nimesababishaje kutendewa nilichotendewa. Na kama unajihesabia haki zaidi na Huoni mapungufu yako basi itakuwa ngumu kwako wewe kusamehe.
Tunasamehe kwa sababu:-
1. Nasi tunahitaji kusamehewa.... Maana tunaendelea kukosea maishani mwetu. Maandiko yanatudai ili Mungu wetu atusamehe nasi twapaswa kusamehe.
2. Kwa ajili ya afya yetu. Grudges au machungu na hasira ni mlango wa magonjwa yasioambukiza kama msongo, shinikizo la damu, sukari, madonda tumbo na hata mawazo ya kujiua.

Ukimchunguza bata humli, ukitafuta sana makosa hukosi maana unakuwa na darubini inayokuza hata tuvitu tudogo. Tumia darubini hiyo kutafuta uzuri wa huyo aliyekukosea as sure as sunshine utauona uzuri wake. Tumia hiyo hiyo darubini kutafuta mapungufu yako, pia utayaona na yatakunyenyekeza utatumia muda wa kutosha kufanya toba na kuwaza jinsi gani utakuwa mtu bora kuliko kuwazia mapungufu ya wengine.

Mungu akusaidie.
 
Acha kuwa na marafiki. Ishi pekee yako kama mimi.
 
waone kama binadamu wa kawaida tuu, pia ona kama watu ulio wazidi uwezo wa kufikilia, maana anaye kukwaza malanyingi ni mtu mwenye uelewa mdogo mpumbavu usije ukawajibu ukafanana na upumbavu wao!
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…