Nahitaji msaada, kichwa kinanisumbua mno

mysara2011

Member
Sep 28, 2017
69
84
Jamani nisaidieni mwenzenu yani kuna mda naumwa kichwa mpaka nahisi navurugwa na ukizingatia nimeenda hospital nimepima vipimo vingi hakuna ugonjwa mpaka kuna kipindi nikahisi may be nimeukwaa nako nikapima nikakutwa sina tatizo.Plz nisaidieni hata dawa za mitishamba zinazotibu nitashukuru maana hii too much nami nachoka kulalamika daily naumwa maana inakuwa as if nafanya maigizo kuna mtu alinishauri ninywe mlonge lakini nao haujanisaidia plz msaada wenu kwa anayejua tiba.
 
Mwamini yesu kama bwna na mokozi wa maisha yako nawe utaokoka nakuwa kiumbe kipya 2koritho 5:17 hapo unaweza kujiombea mwenyewe kwa Mungu atakuponya kabisa, hataukiombewa na mtu mwingine utapona. Vinginevyo utapoteza fedha nyingi hospital na kwawaganga wa kienyeji. Tubu dhambi zako mkuu anza maisha mapya ndani ya Yesu magonjwa ya ajabu ajabu itakuwa historia kwako.
 
Wanasema ukiona kichwa kinakuuma sana basi ujue sehemu ya mwili wako kuna tatizo.
 
Pole sana Mkuu, Hospitali zipi ulienda? Uliwaona madaktari bingwa wa mfumo wa fahamu(Neurologists)?
Nilipimwa huku Dodoma general na benjamin ila kote naonekana sina shida kwa dar niliwahi pimwa mwananyamala full blood picture ila kote naonekana sina tabu ila daktari wa mambo hayo ulonambia sijawahi onana naye hapa nafikiria tu niende kupiga X-ray ya kichwa maana naona inakuwa too much.
 
Aiseee pole sana sana jamani....kwa kweli hata mimi kuna ndugu yangu mmoja anaumwa sana sana na kichwa muda mrefu more than 15years,
amepimwa vipimo vyote Dar.X-RAY,MRI,full blood picture Hakuna kitu,now nimeenda kwa dawa za mitishamba (Asili) sio juju please...sio mfuasi wa hayo mambo,nataka nione itakuwaje...kwa herberlist mmoja anaitwa SHARSTRI HERBRLIST Huwa anajitangaza kwenye TV sana,anapatikana Arusha na Dar, Mtaa wa Swahili/sikukuu kariakoo,jaribu pia na huko.Hata FACEBOOK Unaweza mpata.kama sijakosea jina lake.
 
Ahsante ndugu yangu ngoja nitamtafuta japo sitaki awe wa matunguri
 
Pole sana. Wakati mwingine kuumwa kichwa kunasababishwa na msongo wa mawazo. Kutumia muda mwingi kuwaza jambo au tatizo linalokusibu linachingia maumivu ya kichwa.

Hebu wakati ukiendelea kutafuta tiba jaribu ku-relax, acha kuwaza sana kwa muda mrefu, kunywa maji ya kutosha na tazama pia wingi wa damu katika mwili wako.

Kama una kawaida ya kutoa damu na hukutoa kwa muda mrefu, wingi wa damu unaweza changia tatizo.
 
vp shughuli zako,unywaji wa maji,jee unapata muda wa kupumzika wa kutosha,vp lifestyle yako mawazo nk,macho yako ni salama,kuna muda maumivu au matatizo yako katika macho yanaweza pelekea maumivu ya kichwa
 
Inapotokea mtu akawa,anaumwa kichwa mara zote hutokea ikawa ama,Contents ndani ya kichwa that is Ubongo na mishipa ya damu au kifuniko cha ubongo yaani Fuvu (skull) au Ngozi ya kichwa haya maeneo ndiyo yanatakiwa kuchunguzwa hadi kupata clue ya kuumwa kichwa
B. *Aina ya maumivu
ni maumivu ya kugonga , au ya kubana , au ya kupwita nk
Je yana sambaa au yapo pale pale ,
Je ninini kinayazidisha na kipi angalau kinaleta nafuu japo kidogo
Upi ni uhusiano wake na uoni (kuhusiana na macho)
Uchunguzi wa shinikizo la damu ukoje ^BP
Wakati upi maumivu ya kichwa yanazidi Asubuhi au mchana
Hali ya usingizi nk ninahakika ikifanywa kiadilifu historia na uhunguzi wa CTScan MRI naam naamini utapata ufumbuzi
Habari za kuokoka kwa kwa jina la yesu au kombe kutakupotezea muda maana hayo hutibu Imani na siyo mwili ambao kiungo kikikatika hata waombezi wakeshe miaka saba kiungo hicho hakirudi ng'oo na hata uende kwa gwjima hutopona maana naye anatembea na dawa na pia nguo
 
Fear or self criticism, kama alivyosema Kata kucha, na wachangiaji wengine angalia social life yako ikoje.
Kuna mwandishi kafafanua aina tatu za kichwa kuuma
1.sick headache-anasema inasababiswa na mfumo mbaya wa mmeng'enyo wa chakula tumboni, au ini kuwa na tatizo, au kuwa mwezini kwa mwanamke
2.bilious headache-Ini kuwa na tatizo, upungufu wa mazoezi mwilini, kula kupita kiasi, anasema ukiweza kubadiri mfumo wa ulaji na maisha ndio tiba, ama sivyo utakuwa na tatizo sugu
3.nervous headache-kufanya kazi kupita kiasi, wasiwasi

Jaribu kunywa chai ya meant kikianza kuuma
 
Nadhani ni vizuri ungepima macho ccbrt. nilikuwa na tatizo hilo kwa miaka mingi ila for now ni historia! mara nyingi matatizo ya macho huchangia kwa kiasi kikubwa kichwa kuuma. anzia hapo ikishindikana ntakuelekeza dawa ya asili.
 
Definetly you are right!
 
Jamani nisaidieni mwenzenu yani kuna mda naumwa kichwa mpaka nahisi navurugwa na ukizingatia nimeenda hospital nimepima vipimo vingi hakuna ugonjwa mpaka kuna kipindi nikahisi may be nimeukwaa nako nikapima nikakutwa sina tatizo.Plz nisaidieni hata dawa za mitishamba zinazotibu nitashukuru maana hii too much nami nachoka kulalamika daily naumwa maana inakuwa as if nafanya maigizo kuna mtu alinishauri ninywe mlonge lakini nao haujanisaidia plz msaada wenu kwa anayejua tiba.
Kama upo jijini Dar nenda kanunuwe kitumbini Lozi aka (Almond) nusu kilo uw eunakula kila siku Lozi 12 kichwa chako kitapona.

DAWA YA MARADHI YA KICHWA.jpg
 
Back
Top Bottom