Nahitaji mfadhili nina mabwawa matatu ya samaki

Chililo

Senior Member
Joined
Mar 22, 2013
Posts
150
Reaction score
114
Wadau, Habari za leo.

Mimi ni mfugaji wa samaki, tayari nina mabwawa matatu ya samaki na nimeshaweka vifaranga vya samaki ambavyo vina miezi minne. mabwawa yangu ni makubwa na mazuri sana. changamoto ninayokutana nayo ni namna ya kupata chakula cha kuwalisha hawa samaki/ Hivyo naomba kupata mtu wa kunifadhili chakula cha kuwalisha hawa samaki, ambaye tutaingia naye Mkataba.
Naamini hapa Jukwaani nitawapata. Namba yangu ni 0769555850.
karibuni sana wadau
 
Unakosa chakula cha samaki? Pumba ndoo moja samaki kwenye bwana moja wanaweza kula wiki moja na mabaki ya chakula huko mahotelini.

Katika ufugaji wa samaki chakula ndio gharama nafuu kuliko kitu kingine
 
Kipi ni ghali?
 
Mkuu kama una sehemu nzuri panda mchicha.
Mchicha ukikua utakuwa unavuna chemsha kidogo kwenye sufuria watilie hao samaki.
Walishe pumba pia.
Pumba pia zichemshe kabla ya kuwapa.
 
Pia unaweza kwenda kwa wafanyabiashara wa dagaa masokoni unaongea nao namna ya kupata mabaki ya dagaa yale chenga ambazo haziuziki ni bei nafuu na ni chakula kizuri sana kwa samaki wako
 
Unakosa chakula cha samaki? Pumba ndoo moja samaki kwenye bwana moja wanaweza kula wiki moja na mabaki ya chakula huko mahotelini.

Katika ufugaji wa samaki chakula ndio gharama nafuu kuliko kitu kingine
awalishe mapumba tu uone kama hawatadumaa aingie hasara kubwa.chakula nacho gharama aisee.investment kubwa kama hizo na gharama zinakua kubwa pia.
 
Pia unaweza kwenda kwa wafanyabiashara wa dagaa masokoni unaongea nao namna ya kupata mabaki ya dagaa yale chenga ambazo haziuziki ni bei nafuu na ni chakula kizuri sana kwa samaki wako
kama anafuga kibiashara asifuate ushauri wako.
 
nenda pugu edeni wanatengeneza chakula kizuri ,jaribu kuongea na yule Mzee anaweza kukuelewa akakupa mifuko kadhaa.umebakisha mienzi miwili uvune
 
Please usijaribu kuwalisha saamaki vyakula visivyokuwa na recommended quality and quantity, hapa lazima ufanye feed formulation katika recommended ratio.
Kama utahitaji msaada huo ktk investiment yako tuwasiliane
0755500814
 
Napenda sana hii project wacha nitafute mtaji nitakutafuta mtaalam uliyeweka no yako hapa
 
Pia unaweza kwenda kwa wafanyabiashara wa dagaa masokoni unaongea nao namna ya kupata mabaki ya dagaa yale chenga ambazo haziuziki ni bei nafuu na ni chakula kizuri sana kwa samaki wako
ni kizuri ila inategemea kama maji yame simama tu sehemu moja akiweka mabaki ya dagaa mara nne tu maji huchafuka sana na kusababisha samaki kukosa oxygen atajuta kama maji yanaingia na kutoka sio mbaya!!!
 
Back
Top Bottom